James Paige Morrison (amezaliwa tar. 21 Aprili 1954) ni mwigizaji wa filamu na tamthilia kutoka nchini Marekani. Alizaliwa mjini Bountiful Utah, ni mtoto wa kiongozi wa maofisa,[1] na alikulia mjini Anchorage, Alaska, Marekani.

James Morrison

Amezaliwa James Paige Morrison
21 Aprili 1954 (1954-04-21) (umri 70)
Bountiful, Utah, Marekani
Ndoa Riad Galayini
(1995–hadi leo)
Tovuti rasmi

Katika vipindi vya TV, Morrison amepata kuonekana katika mfululizo wa Frasier, The X-Files, JAG, Murder She Wrote, The West Wing na Six Feet Under.

Hivi karibuni amepata kushika nafasi katika mfululizo wa TV wa 24. Humo alicheza kama mkurugenzi wa CTU na alitumia jina la Bill Buchanan. Alianza kama nyota mgeni katikati ya msimu wa nne (2005), na akaja kuwa katika orodha ya wahusika wakuu katika msimu wa tano, sita, na saba (2006, 2007, 2009), hadi pale uhusika wake ulipokuja kuuawa.

Yeye na mkewe wanaishi mjini Los Angeles na mtoto wao wa kiume, Seamus, ambaye alizaliwa mnamo mwaka wa 1999.

Filamu/TV hariri

  • Space: Above and Beyond (1995) kama Lt. Col. Tyrus Cassius "T.C." McQueen
  • Freedom (2000) kama Colonel Tim Devon
  • The One (2001) kama Officer Bobby Aldrich
  • Catch Me If You Can (2002) kama Kauzasura, Rubani wa Am
  • CSI: Miami (2003) kama Charles (sehemu ya 1 - "Grand Prix")
  • 24 (2005 - 2009) kama Bill Buchanan
  • Revenge (2012) kama Gordon Murphy
  • Numb3rs (2007) kama Commander Chris Frederickson (sehemu ya 1 - "In Security")

Marejeo hariri

Viungo vya Nje hariri

  Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani wa Marekani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu James Morrison kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.