Bill Buchanan
Bill Buchanan ni jina la uhusika wa kipindi cha televisheni cha Kimarekani maarufu kama 24. Uhusika unachezwa na James Morrison. Humu kacheza kama Mkurugezi wa Kitengo cha Kuzuia Ugaidi cha Los Angeles (CTU), kuanzia msimu wa nne hadi wa sita, pale alipolazimishwa ajiuzuru.
Bill Buchanan | |
---|---|
muhusika wa 24 | |
James Morrison kama Bill Buchanan | |
Imechezwa na | James Morrison |
Misimu | 4, 5, 6, 7 |
Maelezo |
Katikati ya Msimu wa 5 na 6, amemwoa Karen Hayes.[1] Amerudi tena katika msimu wa 7, anafanya kazi kama kachero wa kujitegemea juu ya kufichua njama za magaidi katika serikali kuu. Yeye, Tony Almeida, Michelle Dessler, David Palmer, na Mike Novick wamefanya mpango wa kuongopea kifo cha Jack Bauer ili asitiwe kizuizini na serikali ya nchi ya China kwa kosa la kuvamia ubalozi wa China kinyume cha sheria.
Marejeo
hariri- ↑ Owen, Rob. "Supporting players get to shine", Pittsburgh Post-Gazette, 15 Aprili 2007. Retrieved on 2008-07-08.
Viungo vya Nje
hariri- Character biography Ilihifadhiwa 20 Januari 2009 kwenye Wayback Machine. on the official 24 website