Jamestown (St. Helena)

(Elekezwa kutoka Jamestown, Saint Helena)


Jamestown ni bandari na mji mkuu wa eneo la ng'ambo la Uingereza linaloundwa na visiwa vidogo vya Saint Helena, Ascension na funguvisiwa la Tristan da Cunha. Mji uko kisiwani St. Helena katika bahari ya Atlantiki takriban km 1.868 kutoka pwani ya Angola. Idadi ya wakazi inakaribia 1,000.

Jamestown
Nchi Saint Helena
Jamestown mwaka 1970 inavyoonekana kutoka baharini
Jamestown kisiwani Saint Helena.

Mji wenyewe ni hasa barabara moja yenye nyumba za aina ya ujenzi wa kikoloni cha Kiingereza.

Historia

hariri

Jamestown ilianzishwa mwaka 1659 na Kampuni ya Kiingereza ya India ya Mashariki. Miaka ya nyuma bandari ya Jamestown ilikuwa kituo muhimu cha safari za jahazi kubwa kati ya Uingereza, Afrika Kusini na India. Jina limetokana na jina la mfalme James II wa Uingereza na Uskoti (James VII kama mfalme wa Uskoti).

Zamani wafanyabiashara wengi walipeleka dhahabu yao hadi St. Helena kwa sababu kisiwa kilikuwa na sifa ya kuwa mahali pa usalama kwa kutunza dhahabu. Haya yote imepungua hadi kupotea kabisa kwa sababu za mabadiliko ya teknolojia za benki na pia ya usafiri. Leo hii kuna meli tu ya RMS St Helena inayofika takriban mara 2 kwa mwezi ikitumia siku 4-5 kwa ajili ya safari hadi Afrika Kusini. Idadi ya wakazi wa Jamestown imeendelea kupungua.

Viungo vya Nje

hariri
  • "St Helena - Jamestown". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-06-04. Iliwekwa mnamo 2006-12-16.