Jani Allan
Jani Allan alizaliwa tarehe 11 Septemba mwaka 1952) ni mwanahabari, mwandishi na mtangazaji wa Afrika Kusini. Alikuwa miongoni mwa watu mashuhuri wa kwanza kwenye vyombo vya habari kwenye miaka ya 1980 na miaka ya 1990.
Mnamo mwaka 1980, Allan alikuwa mwandishi wa safu wa gazeti la Sunday Times, gazeti lenye mzunguko mkubwa zaidi kwa wiki huko Afrika kusini. Alikuwa mwandishi safi aliyesomwa zaidi kwa muongo mmoja akichapisha safu kama Just Jani, Jani Allan's Week na Face to Face. Akiwa kileleni mwa umaarufu wake, gazeti lilianzisha kura ama uchaguzi wa kutafuta mtu anayependwa zaidi Afrika kusini na aliibuka mshindi.[1] Mwaka 2015,Marianne Thamm wa Daily Maverick alimuelezea Allan kama mwandishi mwenye ushawishi zaidi nchini humo.
Baadaye Allan alikuwa mada ya kutamaniwa kwenye vyombo vya habari juu ya mahusino yake alifanya mahojiano na, Eugène Terre'Blanche. Allan alikana vilivyo madai ya kuwa na mahusiano na alimchukulia hatua Terre'Blanche. Allan aliondoka Afrika Kusini pale nyumba yake ilipolipuliwa na wenye mlengo wa kulia mwaka 1989. Allan aliwashitaki na kushinda maafa kutoka kwa makalia mbili za Uingereza zilizorudia madai ya mahusiano yake. Alifungua mashtaka ya kashfa dhidi ya Channel 4 juu ya Makala ya Nick Broomfield ,ya The Leader, His Driver and the Driver's Wife. Broomfield alikana kutoa madai na mashahidi wa pande zote mbili walisafirishwa kutoka Afrika kusini. Allan alishindwa mashataka hayo ambapo Hakimu alikataa kama kuna yeyote aliyeidanganya mahakama.Baada ya hapo alifanya kazi katika gazeti la London bureau.Alirudi Afrika Kusini mnamo mwaka 1996 akiendelea kuchapisha makala katika Sponsored web na akitangaza katika kipindi cha Redio cha Cape talk.Baada ya mapumziko ya muda mrefu alirudi katika fremu za media za Afrika Kusini mnamo mwaka 2013.Mnamo mwaka 2014 alitengeneza kichwa cha habari duniani kote baada ya kuchapisha barua ya wazi iliyomshutumu muuaji Oscar Pistorious.
Maisha ya awali
haririAllan alilelewa na wenza matajiri wenye asili ya Afrika Kusini na Uingereza Johnn Murray Allan na na Janet Sophia Henning akiwa na umri wa mwezi mmoja.[2] Baba mlezi wa Allan aliyekua mhariri wa zamani wa ‘‘the Johannesburg daily’’, alifariki Allan akiwa na umri wa miezi nane. Mama yake alikua mfanya biashara wa vito vya thamani akiwa na duka Randburg. Allan alikuzwa na Hennings na mumewe wa pili, Walter Erick Monteith Fry. Familia iliishi Randburg kabla ya kuhamia Brayanston Sandton. Allan alisoma shule ya msingi ya Franklin D. Rooselt na shule ya msingi ya Blairgowrie
Marejeo
hariri- ↑ Abstracts Weekly Mail.1992
- ↑ Jani het van kleins af fantastiese verbeelding gehad, sê ma Archived 12 Oktoba 2013 at the Wayback Machine Beeld. 27 July 1992