Jihadi ya Kiislamu ya Misri

Jihadi ya Kiislamu ya Misri au Al-Jihad ya Misri (Ar. الجهاد الإسلامي المصري‎ aljihad alislami almasri) ni kundi lililoanzishwa nchini Misri. Mwanzoni ilitaka kupindua serikali ya Misri na kuanzisha dola la Kiislamu kulingana na mawazo yake kuhusu Uislamu na jihadi. Baadaye ilipanusha shabaha zake kulenga pia dola la Israeli na Marekani.

Kundi lilijiita lenyewe Jihadi ya Kiislamu الجهاد الإسلامي na Jeshi la ukombozi wa mahali patakatifu.[1] Lilianza shughuli zake katika dekadi ya 1970. Lilitangazwa marufuku na Umoja wa Mataifa kama kundi linaloshirikiana na Al Qaida. [2] Linaitwa "Jihadi ya Misri" kwa kuitofautisha na vikundi vingine vinavyotumia pia jina la "Jihad". Mwaka 2001 Al Qaida na mabaki ya Jihadi ya Kiislamu ya Misri waliungana kwa jina la 'Qaida al-Jihad'.[3]

Uuaji wa Rais Anwar Sadat

hariri

Tendo la kwanza la kundi lililojulikana kimataifa lilikuwa shambulio dhidi ya rais wa Misri Anwar Sadat mwaka 1981 walipofaulu kumwua. Washiriki na marafiki wengi walikamatwa na kuhukumiwa lakini wale wa ngazi ya chini waliachishwa baada ya miaka kadhaa wakaondoka Misri wakienda Pakistan na Afghanistan kujiunga na vita ya kupambana na uvamizi wa Umoja wa Kisovyeti katika Afghanistan.

Afghanistan

hariri

Huko Afghanistan walishirikiana na mujahidin kutoka Uarabuni walioongozwa na Osama bin Laden. Watu waliomtembelea bin Laden katika miaka ya 1980 waliona ya kwamba watu kutoka Misri walikuwa karibu naye kila dakika na kumshawishi. Tangu miaka ile Ayman al-Zawahiri alipata nafasi muhimu zaidi na tangu 1991 alikuwa kiongozi wa kundi lililoachana na kiongozi wa awali aliyekaa jela nchini Misri.

Katika Sudan pamoja na bin Laden

hariri

Pamoja na bin Laden Jihadi ya Kiislamu ya Misri ilipata kimbilio kipya huko Sudani. Kutoka hapa waliendelea kupanga mashambulio dhidi ya wawakilishi wa serikali ya Kairo. 1993 walijaribu kumwua waziri wa mambo ya ndani na baadaye waziri mkuu kwa mabomu yaliyobebwa na wanajihadi waliojirusha pamoja na mabomu lakini waliua tu walinzi wa wanaisasa hao pamoja na watu raia waliopita tu.

Mwaka 1995 wanajihadi walijaribu kumwua rais mpya wa Misri Hosni Mubarak aliposhirki kwenye mkutano wa Umoja wa Muungano wa Afrika lakini walishindwa. Serikali ya Misri ikajibu kwa kutafuta vikali watu watu walioweza kuwa na uhusiano na kundi. Hapo msingi wake nchini iliharibika na kunda likategemea zaidi pesa za Osama bin Laden.

Hatua zilizochukuliwa dhidi ya Sudan iliyowapa magaidi nafasi ya kuwa wageni iliongeza shindikizo dhidi yao. Viongozi walipoamua kuwaua dhidi ya ombi la serikali ya Sudani vijana wadogo walioshtakiwa kushirikiana na polisi ya siri ya Misri ilileta azimio la Sudan kuwafukuza wanajihadi nchini.

Kurudi Afghanistan

hariri

Pamoja na Osama bin Laden walirudi Afghanistan walipopata nafasi katika maeneo chini ya Taliban. Al-Jihad ikaendelea na mipango kama shambulio dhidi ya ubaolzi wa Misri nchini Pakistan ya 1995 walipouawa watu 16. Mbinu wa tendo hili lilikuwa kielelezo kwa mashambulio ya kigaidi ya 7 Agosti 1998 katika Afrika ya Mashariki dhidi ya balozi za MArekani huko Nairobi na Dar es Salaam.

Maungano na Al Qaida

hariri

Watu wa Al-Jihad waliendelea kuchukua nafasi muhimu katika Al Qaida ya bin Laden ingawa kundi bado liliendelea na mipango yake ya pekee. Mwaka 2001 vikundi viwili viliungana rasmi kabla ya mashambulio ya kigaidi ya 11 Septemba 2001 katika Marekani.

Marejeo

hariri
  1. Global Briefings, Issue 27, Septemba 1998, “Osama Bin Laden tied to other fundamentalists”.
  2. Affiliates of al-Qaeda and the Taliban, United Nations Security Council Committee 1267
  3. Lawrence Wright 2002. The New Yorker. The Man Behind Bin Laden Archived 24 Februari 2011 at the Wayback Machine.