Jiwe mchanga (kwa Kiingereza: sandstone) ni aina ya mwamba mashapo. Linaundwa na mchanga uliogandamizwa, hivyo madini ndani yake ni hasa shondo na felispa.

Jiwe mchanga jekundu.

Jiwe mchanga ni mwamba thabiti ambayo hailikwi kirahisi, pia si ngumu mno, hivyo hutumiwa kwa ujenzi katika nchi nyingi.

Jiwe mchanga linabadilika kuwa kwasiti kama inaathiriwa na shinikizo kubwa, kwa mfano chini ya matabaka ya ardhi au kama linalala chini ya milima.

Asili hariri

Jiwe mchanga huundwa katika hatua mbili. Kwanza, mchanga unakaa na kuunda tabaka la mashapo.

Baada ya matabaka ya mashapo mapya zaidi hukusanya juu yake, hili tabaka la mashapo linagandamizwa na uzito wa matabaka ya juu yakiimarishwa kuwa jiwe.

Oksidi ya chuma mara nyingi hufanya jiwe mchanga liwe na rangi nyekundu.

Tanbihi hariri

  Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Jiwe mchanga kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.