John Herald

Mwanamuziki wa Mareakani (1939-2005)

John Herald (Septemba 6, 1939 - Julai 18, 2005) alikuwa mtunzi wa nyimbo kutoka nchini Marekani, mwanamuziki na mwanachama wa kundi la The Greenbriar Boys . [1] [2]

Wasifu

hariri

Herald alizaliwa huko Manhattan mnamo 1939, baba yake akiwa mshairi wa Armenia Leon Serabian Herald. Ilikuwa ni kupitia kwake ambapo Herald alionyeshwa kwa mara ya kwanza maonyesho ya moja kwa moja na waimbaji wa muziki wa blues na hadithi za kitamaduni Lead Belly na Woody Guthrie . Akiwa katika kambi muda wa kiangazi mwaka wa 1954, Herald alivutiwa na Pete Seeger . Wakati akiwa shuleni Manumit, alikua msikilizaji mzuri wa kipindi cha redio cha Don Larkin cha aina ya muziki wa bluegrass, na akaanza kuhudhuria mubashara upigaji wa gitaa kutoka kwa Bob Dylan na Rory Block .

Mnamo 1958, Herald aliunda kundi la The Greenbriar Boys, pamoja na Bob Yellin (mpiga banjo) na Paul Prestopino (mpiga mandolin). Mwaka uliofuata, Eric Weissberg (mpiga mandolin na fidla), alichukua nafasi ya Prestopino, na Weissberg nafasi yake ikachukuliwa na Ralph Rinzler (mpiga mandolin) na kuunda kundi bora na lenye mafanikio zaidi. Herald alikuwa mpiga gitaa na mwimbaji . Watatu hao mara nyingi walicheza onyesho la huko Kijiji cha Greenwich, lakini walijulikana vya kutosha kuwa kundi la kwanza la kanda ya Kaskazini kushinda shindano la Union Grove la upigaji Fidla, ambapo The Greenbriar Boys walisainiwa lebo ya Vanguard, ambao walitoa rekodi tatu. Mnamo 1969, Linda Ronstadt alirekodi wimbo wa Herald "High Muddy Water." Miaka miwili hapo awali, alitengeneza nyimbo na kuingiza sauti akiwa na Mike Nesmith, katika nyimbo ya "Different Drum" ambayo ilivuma sana katika bendi yake ya Stone Poneys .


Rekodi ya mwisho ya Herald ilikuwa Roll On John mnamo 2000. Alikuwa akifanya kazi kwenye nyenzo mpya ya muziki 2005, mnamo Julai 19, mwili wake ulipatikana nyumbani kwake huko West Hurley, New York . Polisi wa jimbo hilo walishuku kujiua, ingawa hakuna sababu rasmi iliyotolewa kuhusu kifo chake.

Marejeo

hariri
  Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu John Herald kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.