Joseph Garang

Mwanasiasa wa Sudani ya kusini

Joseph Ukel Garang Wel (28 Julai 1932- 1971) alikuwa mwanasiasa wa Sudan, upande wa Sudani Kusini.

Elimu na TaalumaEdit

Garang alisoma shule ya St. Antony's Bussere (1944-1948) na Rumbek Secondary School (1949-1953). Mnamo mwaka 1957,alikuwa mwanamume wa kwanza Msudani kupata shahada ya sheria wakati akihitimu katika chuo kikuu cha Sudani cha University of Khartoum.

Muda mfupi baada ya kuhitimu masomo yake, alikataa kuwa mwanasheria mkuu na badala yake alitaka kufanya kazi ya kujitolea kama mwanasheria huku akiendeleza kazi yake ya kuwa mwanasiasa.[1][2]

SiasaEdit

Joseph Garang alikuwa mwanachama wa chama cha siasa cha Sudanese Communist Party, na kuhudumu kama waziri katika serikali ya watu wa Sudan.[3]

Mnamo mwezi Julai mwaka 1971, Garang pamoja na watu wengine, waliuliwa kutokana na kupatikana na tuhuma ya kula njama za uhaini wa kimapinduzi dhidi ya serikali ya rais Gaafar Nimeiry.[4]

MarejeoEdit

  1. Kuyok, Kuyok Abol (2015-09-04). South Sudan: The Notable Firsts (in en). AuthorHouse. ISBN 9781504943468. 
  2. "Joseph Ukel Garang Wel: The Firebrand Marxist and Intellectual of South Sudan", PaanLuel Wël Media Ltd - South Sudan, 2018-07-14. (en-US) 
  3. Natsios, Andrew S. (2012-03-23). Sudan, South Sudan, and Darfur: What Everyone Needs to Know® (in en). Oxford University Press. ISBN 9780199831371. 
  4. Communist Leader Sentenced By Military Court, Washington Post, 28 July 1971
  Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Joseph Garang kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.