Joseph Kamaru

(Elekezwa kutoka Joseph kamaru)

Joseph Kamaru (1939 - 3 Oktoba 2018) alikuwa mwanamuziki wa benga na pia nyimbo za kumsifu Mungu.

Kamaru alikuwa mtunzi mahiri aliyeweza kutunga nyimbo nyingi na kuuza takribani rekodi nusu milioni. Nyimbo zake zilikuwa na maudhui ya mapenzi, jinsi ya kuishi vizuri, kuhusu watoto kutumiwa vibaya kimapenzi na wazee pamoja na kuwakashifu wanasiasa.

Utoto wake

hariri

Kamaru wa Wanjiru, kama alivyopenda kujiita, alizaliwa Kangema, kaunti ya Murang'a.

Mwaka 1957 alihamia Nairobi alipopata kazi ya utopasi. Pia alifanya kazi ya nyumba iliyomwezesha kununa gitaa ya kwanza.

Alianza kufuatilia ndoto yake ya muziki mwaka 1965.

Kazi ya muziki

hariri

Wimbo wa kwanza wa Kamaru uliovuma sana ni Celina aliouimba na dada yake. Nyimbo zake nyingi zilikuwa na jumbe za siasa na aliweza kuwa na mkabala mzuri na rais wa kwanza wa Kenya. Hata hivyo, walitofautiana alipouliwa Josiah Mwangi Kariuki (JM) na Kamaru akautoa wimbo wa kukaripia kitendo kile.

Kamaru pia walikua na mkabala mwema na rais wa pili Daniel Toroitich Arap Moi na aliweza kutunga wimbo kwa jina 'Safari ya Japani' baada ya kuzuru nchi ile na Moi mwaka 1980.

Ugonjwa na kufariki

hariri

Kamaru alifariki tarehe 3 mwezi wa Oktoba 2018 baada ya kuugua ugonjwa wa Parkinson. Alifariki akiwa na umri wa miaka 79.

  Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Joseph Kamaru kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.