Josiah Mwangi Kariuki
Josiah Mwangi Kariuki (aliitwa na watu wengi “J.M.”; 21 Machi 1929 - 2 Machi 1975) alikuwa mwanasiasa wa Kenya wakati wa uongozi wa Jomo Kenyatta. Yeye alikuwa katika nafasi tofauti za serikali kutoka mwaka 1963, wakati Wakenya walipata uhuru, mpaka 1975, alipofariki. Alikuwa na wake watatu na watoto wengi.
Josiah M. Kariuki | |
Ukumbusho wa Josiah Kariuki katika eneo la kifo chake. | |
Muda wa Utawala 1974 – 1975 | |
Rais | Jomo Kenyatta |
---|---|
tarehe ya kuzaliwa | Kibati-ini, Mkoa wa Rift Valley | 21 Machi 1929
tarehe ya kufa | 2 Machi 1975 (umri 45) Nairobi, Kenya |
Maisha na elimu
haririKariuki alizaliwa katika mji wa Kabati-ini katika mkoa wa Rift Valley. Jina la baba yake lilikuwa Kariuki Kigani, na jina la mama yake lilikuwa Mary Wanjiku. Yeye alikuwa na dada watano, na Josiah alikuwa mvulana pekee. Wazazi wake walilazimishwa kuhama mji wao mwaka wa 1928 kwa sababu walihitaji kufanya kazi kwenye shamba la Mzungu. Familia nyingine walilazimishwa kufanya kazi ili kupata pesa.
Yeye alikuwa na wakati mgumu kujaribu kwenda shuleni kwa sababu hakuwa na pesa.
Katika mwaka wa 1946 yeye alishinda mchezo wa kamari wa mbio za farasi. Yeye alitumia hiyo pesa kwa kulipia elimu yake. Alikwenda shule iliyoitwa Evanson Day School kwa elimu ya msingi na kwa elimu ya sekondari alikwenda shule iliyoitwa King’s College Budo katika mji wa Wakiso nchi ya Uganda.
Siasa
haririKariuki alianza kazi ya siasa katika mwaka 1946 badaa ya kusikiliza hotuba ya Kenyatta kuhusu njia ambayo serikali ilinyanyasa wananchi asili. Baada ya Kariuki kumaliza elimu ya sekondari, alijiunga na muungano wa mapinduzi katika Kenya. Wakati huo Kenya ilikuwa na hali ya dharura, ndiyo maana yeye alijiunga na muungano wa mapinduzi. Kikundi hicho kiliitwa Mau Mau. Yeye alisaidia Mau Mau na majukumu mbalimbali na alikamatwa kuwa sababu hiyo.
Aliachiliwa baada ya miaka saba mwaka wa 1960. Baada ya kuachiliwa, alifanya kazi na Jomo Kenyatta akawa katibu wake kutoka 1963 mpaka 1969. Kariuki na Kenyatta walianza kutokubaliana kuhusu kanuni ya kisiasa. Baada ya kuachiliwa yeye alianza Jumuiya ya Kitaifa ya Kenya (KANU) katika sehemu ya Nyeri. Kariuki alichaguliwa kwa mbunge kutoka 1974 mpaka 1975. Serikali ilijaribu kubatilisha uchaguzi wake kwa sababu yeye alikuwa maarufu, labda maarufu kuliko Kenyatta.
Kifo
haririAlipatikana amefariki tarehe 2 Machi 1975. Habari ya kifo chake ilipoenea, yalianzishwa maandamano katika mji mkuu na kutoka wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi. Polisi walikuja na walisimamisha maandamano yao. Chuo kikuu hicho kilifungwa kwa muda mrefu. Bunge liliunda kamati ili kuchunguza kifo cha Kariuki. Wao walipewa watu wengi kwa uchunguzi. Mwishowe hawakupata mtu yeyote kuwajibika.
Kitabu chake
haririYeye aliandika kitabu kabla hajafa, kilichoitwa “Mau Mau Detainee” kwa Kiingereza, kuhusu wakati wake katika kambi za kizuizini kutoka 1953 mpaka 1960, wakati wa muungano wa mapinduzi kwa uhuru katika Kenya.
Marejeo
hariri- https://www.bbc.com/news/world-africa-31817667
- https://www.encyclopedia.com/education/news-wires-white-papers-and-books/kariuki-j-m
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Josiah Mwangi Kariuki kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |