Josh Giddey

Mchezaji wa mchezo wa mpira wa kikapu wa Australia

Joshua James Giddey (alizaliwa 10 Oktoba 2002) ni mchezaji wa mpira wa kikapu wa kulipwa kutoka Australia anayechezea timu ya Chicago Bulls ya Chama cha Mpira wa Kikapu wa Marekani(NBA). Alichaguliwa na timu ya Oklahoma City Thunder kwenye uteuzi wa drafti ya Chama cha Mpira wa Kikapu wa Marekani ya mwaka 2021 nafasi ya sita, Giddey ni mchezaji mdogo zaidi katika historia ya Chama cha Mpira wa Kikapu wa Marekani kurekodi triple-double, akiwa na umri wa miaka 19 na siku 84. Pia alikuwa mchezaji chipukizi wa kwanza tangu Mwanachama wa Hall of Fame Oscar Robertson mwaka 1961 kurekodi triple-double tatu mfululizo.[1]

Giddey Mwaka 2022

Maisha ya awali na kazi

hariri

Giddey alizaliwa Melbourne kwa wazazi ambao ni wachezaji wa mpira wa kikapu wa kulipwa.[2] Baba yake, Warrick, alikuwa mchezaji wa mpira wa kikapu na alikuwa mchezaji wa muda mrefu wa timu ya Melbourne Tigers nchini Australia.[3] Mama yake, Kim, alikuwa mchezaji wa timu ya Tigers katika Ligi ya Taifa ya Mpira wa Kikapu ya Wanawake (kwa kiingereza: Women's National Basketball League).[4]

Marejeo

hariri
  1. "Aussie matches feat last seen in NBA 61 years ago". Nine (kwa Kiingereza). 2022-02-17. Iliwekwa mnamo 2024-06-23.
  2. "Australian basketball's next big thing is set to jump from the NBL to the NBA", ABC News (kwa Australian English), 2021-03-13, iliwekwa mnamo 2024-06-23
  3. Ayush G. "Josh Giddey: The road so far for Melbourne's next great prospect". pickandroll.com.au (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-06-23.
  4. Roy Ward (2021-01-16). "NBA prospect Giddey learns big lessons in NBL". The Sydney Morning Herald (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-06-23.