Julie Manning
Julie Manning (alizaliwa Morogoro, 24 Januari 1939) alikuwa mwanasheria, hakimu na mwanasiasa wa Tanzania. Alikuwa mwanamke wa kwanza kusoma sheria nchini Tanzania, akawa Jaji wa Mahakama Kuu kabla ya kutumikia kama Waziri wa Sheria kutoka mwaka 1975 mpaka 1983.
Julie Cathrine Manning | |
Amezaliwa | 24 Januari 1939 Tanzania |
---|---|
Nchi | Tanzania |
Kazi yake | Mwanasheria, Hakimu na Mwanasiasa |
Cheo | Waziri wa Sheria |
Kipindi | 1973 - 1975 |
Akafuatiwa na |
Maisha
haririKatika mwaka 1963 Julie Manning alikuwa mwanamke wa kwanza kusoma sheria katika Chuo Kikuu cha Afrika Mashariki. Baadae alisoma Sheria na kuwa "Law draughtswoman" katika ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.[1]
Mwaka 1973 alichaguliwa kuwa Hakimu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, alifanywa mwanamke wa kwanza kuwa Hakimu wa Mahakama kuu katika Afrika Mashariki na kati.[2] Mwaka 1975 alichaguliwa kuwa Waziri wa Sheria, kumfanya awe mmoja wa wanawake wawili wa kwanza kutumikia Baraza la mawaziri Tanzania.[3]
Jaji Joseph Warioba alikuwa Waziri wa Sheria mwaka 1983 baada ya Bi. Manning kutolewa katika wizara hiyo na kuwa mshauri katika Ubalozi wa Tanzania huko Washington.[4]
Marejeo
haririViungo vya nje
hariri- Tovuti ya Bunge la Tanzania
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Julie Manning kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |