FORD-Kenya

(Elekezwa kutoka Ford-Kenya)

FORD-Kenya (pia: FORD-K) ni chama cha kisisasa nchini Kenya. Jina ni kifupi cha Forum for the Restauration of Democracy-Kenya. FORD-Kenya ilianzishwa 1992 baada ya farakano ya harakati ya FORD ya pamoja.

Chanzo katika Ford ya awali hariri

FORD (Forum for the Restauration of Democracy) ilikuwa harakati ya kisiasa tangu 1991 iliyopigania kuruhusiwa kwa vyama vingi na demokrasia wakati wa mfumo wa chama kimoja na utawala wa KANU nchini Kenya. Rais Daniel arap Moi alilazimishwa na nchi za nje kukubali uchaguzi wa vyama vingi. Kabla ya uchaguzi wa 1992 FORD ilifarakana kati ya wafuasi wa viongozi Kenneth Matiba kutoka Mkoa wa Kati na Jaramogi Oginga Odinga kutoka Mkoa wa Nyanza. Wafuasi wa Odinga waliunda FORD-Kenya. Wafuasi wa Matiba waliendelea kwa jina la FORD-Asili.

Ford-K ilipata nafasi ya tatu katika uchaguzi wa rais 1991. Kutokana na farakano la upoinzani Moi alirudishwa kama rais.

Farakano ya Raila 1994 hariri

Chama kiliona farakano tena 1994 Odinga alipoaga dunia. Katika mkutano wa chama Michael Wamalwa kutoka Kenya ya MAgharibi alichaguliwa kuwa mwenyekiti mpya akimshinda Raila Odinga mwana wa Jaramogi. Raila aliondoka katika FORD-K na kujiunga na chama kidogo cha National Development Party NDP. Wabunge wengi wa Ford-K kutoka Nyanza walimfuata Raila hivyo chama kilipungukiwa kikawa na nguvu hasa katika Mkoa wa Magharibi kati ya Waluhya.

Katika uchaguzi wa 1997 chama kilipata nafasi ya nne tu baada ya NDP.

Uchaguzi 2002 hariri

2002 Ford-K ilijiunga na harakati ya NARC ikawa sehemu ya maungano yaliyompeleka Mwai Kibaki katika ikulu ya Nairobi. Kiongozi wa chama Michawel Wamalwa alikuwa makamu wa rais lakini alikufa 2003 katika ajali ya ndege. Kiongozi mpya akawa Musikari Kombo.

Baada ya kuvunjwa kwa serikali ya NARC mwaka 2005 FORD-K iliongezwa idadi ya mawaziri wake kuwa 6.

Uchaguzi 2007 hariri

Katika uchaguzi wa 2007 Ford-K ilijiunga na ushirikiano wa PNU wa Mwai Kibaki. Chama kiliona farakano tena kwa sababu New Ford-Kenya ikajitenga chini ya Mukhisa Kituyi. Kwa jumla chama kilishika kiti kimoja bungeni tu na mwenyekiti Musikari Kombo hakurudishwa.