National Development Party of Kenya
National Development Party (NDP) ilikuwa chama cha kisiasa nchini Kenya. Ilikuwa maarufu kama chama cha Waluo hasa tangu 1994 hadi kuungana na KANU mwaka 2001.
Kutokea kwa NDP
haririAwali NDP ilikuwa bila umuhimu lakini mwaka 1994 ilimpokea Raila Odinga aliyeondoka katika chama cha Ford-Kenya baada ya kushindwa kupata uongozi dhidi ya Michael Wamalwa.
Raili alifaulu kuvuta wabunge wengi wa FORD-Kenya kutoka mkoa wa Nyanza. Walipaswa kurudia uchaguzi baada ya kuhama chama lakini walifaulu kupita tena kwa tiketi ya NDP.
Uchaguzi wa 1997
haririKatika uchaguzi wa 1997 NDP ilipata wabunge NDP 21 hasa katika Nyanza kati ya Waluo lakini Raila alifaulu kama mbunge wa Langata mjini Nairobi. NDP ilikuwa chama cha pili cha upinzani baada ya DP.
Ushirikiano katika serikali
haririTangu 2000 NDP ilianza ushirikiano na serikali. Mwezi wa Juni 2001 ushirikiano huu ulikuwa rasmi na mawaziri watatu wa NDP waliingia katika serikali ya KANU. Raila Odinga akawa waziri wa nishati.
Maungano na KANU na farakano
haririMwaka 2001 NDP ikaungana na chama tawala cha KANU na Raila akawa Katibu Mkuu wa chama kilichounganishwa.
Lakini katika Oktoba 2007 farakano kubwa likatokea ndani ya KANU baada ya rais Moi kumteua Uhuru Kenyatta kama mfuasi wake. Raila aliondoka katika KANU akifuatwa na kundi lake la NDP ya awali. Kundi ka NDP liliondoka pamoja na wanaKANU waliosikitika uteuzi wa Uhuru Kenyatta.
Mwisho kamili katika LDP
haririWote kwa pamoja waliingia katika LDP. Baadaye hapakuwa tena na taarifa juu ya NDP. LDP ikaunda harakati ya NARC iliyoshinda uchaguzi wa 2002.