Kahama (mji)
Kahama ni manisipaa[1] iliyo kaskazini magharibi mwa Tanzania na yalipo makao makuu ya wilaya ya Kahama Mjini katika Mkoa wa Shinyanga, wenye halmashauri yake ya pekee hivyo yenye hadhi ya wilaya. Halmashauri ilianzishwa baada ya kugawa Wilaya ya Kahama ya awali.
Kata ya Kahama | |
Nchi | Tanzania |
---|---|
Mkoa | Shinyanga |
Wilaya | Kahama |
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 453,654 |
Mahali ilipo
haririKahama ipo takriban kilomita 109 (sawa na maili 68) umbali kwa barabara kutokea kusini magharibi mwa Shinyanga ambapo makao makuu ya mkoa yanapatikana.[2] pia ni takriban kilomita 536 sawa na maili 333 umbali kwa barabara kutokea kaskazini magharibi mwa Dodoma ambao ndio mji mkuu wa Tanzania.[3]
Idadi ya watu
haririMwaka 2006 ilikadiriwa kuwa na idadi ya watu 36,000.[4]
Katika sensa ya mwaka 2012, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa watu 242,208. [5] na katika ile ya mwaka 2022 walihesabiwa 453,654 [6].
Mji huu ni maarufu kwa uchimbaji wa dhahabu. Pia ni mji wa pili kwa mapato kati ya halmashauri za wilaya, ikitanguliwa na Kinondoni na kufuatiwa na Mufindi.
Tangu 1984 mji umekuwa makao makuu ya dayosisi ya Kahama ya Kanisa Katoliki.
Marejeo
hariri- ↑ JPM uplifts Kahama to municipality status, ippmedia 30.01.2021
- ↑ "Distance Between Kahama And Shinyanga, With Interactive Map". Globefeed.com. Iliwekwa mnamo 20 Novemba 2014.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Map Showing Kahama And Dodoma With Distance Marker". Globefeed.com. Iliwekwa mnamo 20 Novemba 2014.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Estimated Population of Kahama, Tanzania In January 2006". Mongabay.com. 2006. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-11-29. Iliwekwa mnamo 20 Novemba 2014.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Sensa ya 2012, Shinyanga Region - Kahama Town Council
- ↑ https://www.nbs.go.tz
Viungo vya nje
hariri- [http://web.archive.org/20080317142956/http://tecdirectory.tripod.com/dkahama.htm Archived 17 Machi 2008 at the Wayback Machine. Jimbo Katoliki la Kahama]
Kata za Wilaya ya Kahama Mjini - Mkoa wa Shinyanga - Tanzania | ||
---|---|---|
Busoka | Isagehe | Iyenze | Kagongwa | Kahama Mjini | Kilago | Kinaga | Majengo | Malunga | Mhongolo | Mhungula | Mondo | Mwendakulima | Ngogwa | Nyahanga | Nyandekwa | Nyasubi | Nyihogo | Wendele | Zongomera |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Shinyanga bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Kahama (mji) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno. |