Kaisarea Baharini

(Elekezwa kutoka Kaisarea Maritima)

32°30′0″N 34°53′30″E / 32.50000°N 34.89167°E / 32.50000; 34.89167

Magofu ya mji.
Kutoka katika ndege.
Mabaki ya njia ya maji ya Kiroma.
Mahali pa kuonyesha tamthilia.
Nguzo.

Kaisarea Baharini (kwa Kigiriki Παράλιος Καισάρεια, Parálios Kaisáreia) ulikuwa mji wa Palestina kuanzia mwaka 10 KK hadi 1265 BK.

Kwa sasa ni sehemu ya Hifadhi ya Taifa la Israeli katika bonde la Sharon[1].

Ulianzishwa na mfalme Herode Mkuu ukawa makao ya liwali wa Dola la Roma aliyetawala Palestina.

Baadaye ukawa kituo muhimu cha Ukristo, ambapo Mtume Petro alibatiza akida Korneli na familia yake (Mdo 10:1-11:18).

Ndipo alipoishi Filipo mwinjilisti (Mdo 8:40) ambaye alimkaribisha Mtume Paulo kwa siku kadhaa (Mdo 21:8-10) katika moja ya nafasi yake ya kupitia mjini huko (Mdo 9:30; 18:22).

Baadaye Paulo alikaa gerezani huko kwa zaidi ya miaka miwili akisubiri kuhukumiwa, mpaka alipokata rufaa kwa Kaisari Nero (23:23; 15:1-13).

Tanbihi

hariri
  1. "Caesarea National Park". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-10-26. Iliwekwa mnamo 2017-10-21.

Marejeo

hariri

Viungo vya nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kaisarea Baharini kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.