Kalenda ya Ethiopia

Kalenda ya Ethiopia (kwa Kiamhari: የኢትዮጵያ ዘመን አቆጣጠር ye'Ityoṗṗya zemen aḳoṭaṭer) ni kalenda rasmi nchini Ethiopia na pia kalenda inayotumiwa na Wakristo walio wengi nchini Eritrea. Asili yake ni kalenda ya Wakopti kwa sababu Kanisa la Ethiopia kwa karne nyingi lilikuwa kama tawi la kanisa la Kikopti la Misri.

Miezi 13 na miaka mirefu

hariri

Kalenda huwa na mwaka wa miezi 13; miezi kamili 12 ya siku 30 na mwezi wa 13 mfupi wa siku 5 yaani jumla siku 365. Kila mwaka wa 4 ni mwaka mrefu ambako mwezi wa 13 huwa na siku 6 yaani siku 366 kwa jumla. Chanzo cha mwaka kinalingana na 11 Septemba ya kalenda ya Gregori (kalenda ya kimataifa), isipokuwa baada ya mwaka mrefu kinalingana na 12 Septemba na tofauti inasawazishwa katika mwaka mrefu wa kalenda ya Gregori.

Tofauti na kalenda ya Gregori utaratibu wa mwaka mrefu kila mwaka wa nne unaendelea bila kituo.

Hesabu ya miaka

hariri

Hesabu ya miaka ni tofauti na mwaka wa Gregori kiasi cha miaka 7-8. Sababu yake ni ykwamba kalenda hii, sawa na ya Wakopti, hufuata makadirio ya mwaka wa kuzaliwa kwake Yesu ambayo ni tofauti kidogo na hesabu ya magharibi inayomfuata Dionysius Exiguus. Kati ya Januari hadi 10/11 Septemba tofauti ni miaka 8, kwa miezi inayobaki tofauti ni miaka 7. Kwa hiyo mwaka 2007 ya kalenda ya kimataifa ililingana na mwaka 2000 wa Ethiopia.

Ge'ez, Kiamhari na Kitigrinya Kikopti Chanzo cha mwaka
katika kalenda ya Gregori
Chanzo cha mwaka
baada ya mwaka mrefu
Mäskäräm (መስከረም) Tut 11 Septemba 12 Septemba
Ṭəqəmt(i) (ጥቅምት) Babah 11 Oktoba 12 Oktoba
Ḫədar (ኅዳር) Hatur 10 Novemba 11 Novemba
Taḫśaś ( ታኅሣሥ) Kiyahk 10 Desemba 11 Desemba
Ṭərr(i) (ጥር) Tubah 9 Januari 10 Januari
Yäkatit (Tn. Läkatit) (የካቲት) Amshir 8 Februari 9 Februari
Mägabit (መጋቢት) Baramhat 10 Machi 10 Machi
Miyazya (ሚያዝያ) Baramundah 9 Aprili 9 Aprili
Gənbot (ግንቦት) Bashans 9 Mei 9 Mei
Säne (ሰኔ) Ba'unah 8 Juni 8 Juni
Ḥamle (ሐምሌ) Abib 8 Julai 8 Julai
Nähase (ነሐሴ) Misra 7 Agosti 7 Agosti
Ṗagʷəmen/Ṗagumen (ጳጐሜን/ጳጉሜን) Nasi 6 Septemba 6 Septemba

Marejeo

hariri
  • "The Ethiopian Calendar", Appendix IV, C.F. Beckingham and G.W.B. Huntingford, The Prester John of the Indies (Cambridge: Hakluyt Society, 1961).
  • Ginzel, Friedrich Karl, "Handbuch der matematischen und technischen Chronologie", Leipzig, 3 vol., 1906-1914

Viungo vya Nje

hariri
  Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kalenda ya Ethiopia kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.