Kanisa la Kiorthodoksi la Ethiopia
Kanisa la Kiorthodoksi la Ethiopia (kwa Kiamhara የኢትዮጵያ:ኦርቶዶክስ:ተዋሕዶ:ቤተ:ክርስቲያን, Yäityop'ya ortodoks täwahedo bétäkrestyan) ni madhehebu ya dini ya Ukristo iliyotawala watu wa jamii ya Waamhara kwa karne kadhaa hadi sasa.
Wakristo hao wanaotaka kuzingatia imani sahihi ni sehemu muhimu katika utamaduni wa Ethiopia na Eritrea[1].
Kwa sasa ni kubwa zaidi duniani kuliko mengine yote ya jamii ya Makanisa ya Kiorthodoksi ya Mashariki, likiwa na waumini milioni 45-50.[2] wengi wao wakiishi nchini Ethiopia,[3] lakini pia Mashariki ya Kati, Ulaya na Amerika.
Historia
haririKanisa la Kiorthodoksi la Ethiopia linaendeleza ushirika na Kanisa la Misri tangu lilipoanzishwa na mtakatifu Frumensyo aliyetumwa na mtakatifu Atanasi, Patriarki wa Aleksandria katikati ya karne ya 4 BK.
Hata hivyo mwaka 1959 lilikubaliwa liwe na Patriarki wake mwenyeji na kujiongoza.
Kalenda
haririKufuatana na mapokeo ya huko Misri, Epifania na Pasaka ni sikukuu muhimu sana, na husherehekewa kwa kufanya mambo kama vile kufunga kula na kucheza.
Pia kuna siku kadhaa katika mwaka ambapo ni mboga za majani pekee na samaki ndio huruhisiwa kuliwa.
Desturi
haririNdoa huweza kuanzishwa au kupangwa wakati mwanamume ana umri wa miaka kumi na..., au ishirini na... Kiutamaduni, wasichana wanaruhusiwa kuolewa wakiwa na umri wa miaka 14 hadi 18, lakini katika karne ya 20, mambo yamebadilika, hivyo sasa umri mdogo kuliko wote wa kuolewa ni miaka 18, na suala hili linasimamiwa na serikali. Ndoa za kiserikali ni nyingi japo pia, wapo watu wanaofunga ndoa katika makani mbalimbali. Na baada ya kufunga ndoa kanisani, suala la talaka halipo na haliwezekani. Kila familia hufanya sherehe ya ndoa baada ya harusi.
Tangu kuzaliwa, padri hutembelea familia kwa ajili ya kumbariki mtoto, na pia kutahiri mtoto kama ni wa kiume. Mama wa mtoto, hutakiwa kukaa ndani kwa siku 40 baada ya kujifungua kama mtoto ni wa kiume na kukaa ndani kwa siku 80 kwa mtoto ni wa kike kabla ya kwenda kanisani kwa ajili ya ubatizo.
Sanaa
haririSanaa ya nchini Ethiopia kwa ujumla imeegamia katika masuala ya dini na michoro ya dini.
Mmoja kati ya michoro mizuri zaidi ya vitu au watu wenye macho makubwa na mara nyingi huwa ni watu wanaohusiana na Biblia.
Tanbihi
hariri- ↑ FDRE States: Basic Information - Amhara Archived 10 Machi 2007 at the Wayback Machine., Population (accessed 26 Machi 2006)
- ↑ "Ethiopia: Orthodox Head Urges Churches to Work for Better World". Iliwekwa mnamo 2006-09-13.
- ↑ Berhanu Abegaz, "Ethiopia: A Model Nation of Minorities" (accessed 6 April 2006)
Marejeo
hariri- Archbishop Yesehaq. 1997. The Ethiopian Tewahedo Church: an Integrally African Church. Winston-Derek Publishers.
- Mikre-Sellassie Gebre-Amanuel. 1993. “The Bible and Its Canon in the Ethiopian Orthodox Church.” The Bible Translator 44/1:111-123.
Viungo vya nje
hariri- Divine Liturgy of the Ethiopian Orthodox Church
- Ethiopian Orthodox Church Directory Archived 20 Novemba 2006 at the Wayback Machine. Directory of Ethiopian Orthodox Churches
- Ethiopian Review's Directory of Ethiopian churches Archived 29 Julai 2016 at the Wayback Machine.
- Ethiopian Religions – Christianity, Islam, Judaism & Paganism Archived 19 Novemba 2020 at the Wayback Machine.
- Bilingual Ethiopian Orthodox Tewahedo Church site – English version
- List of Ethiopian Orthodox Tewahedo Church websites Archived 18 Desemba 2010 at the Wayback Machine.
- Ethiopian Orthodox Tewahedo Church (Ethiopian Orthodox Tewahedo Church -the oldest site)
- Tewahedo Songs & Records
- CNEWA article by Ronald Roberson: Ethiopian Orthodox Tewahedo Church
- Historical Evolution of Ethiopian Anaphoras Archived 4 Julai 2008 at the Wayback Machine.
- Abbink, J. A Bibliography on Christianity in Ethiopia. Leiden: African Studies Centre, 2003 Archived 28 Januari 2018 at the Wayback Machine. (PDF)
- AN INTRODUCTION TO Ethiopic Christian Literature BY J. M. HARDEN, D.D., LL.D. Canon of St. Patrick's, Dublin, 1926 Archived 17 Septemba 2009 at the Wayback Machine.
- Ethiopian Orthodox Tewahedo Church outside of Ethiopia – includes music and preaching
- Ethiopian Crucifixes Gallery
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kanisa la Kiorthodoksi la Ethiopia kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |