Wilaya ya Nkhotakota

Mahali pa Wilaya ya Nkhotakota nchini Malawi

Wilaya ya Nkhotakota ni wilaya mojawapo katika Kanda ya Kati nchini Malawi. Makao makuu yako Nkhotakota. Wilaya ina eneo la km² 4,259 na ina wakazi 395,897. [1] Neno Nkhotakota linamaanisha "kona-kona" katika lugha ya Chichewa. Iko kando ya Ziwa Nyasa inayoitwa hapa Ziwa Malawi.

Vitengo na utawalaEdit

Kuna majimbo matano ya Bunge la Kitaifa huko Nkhotakota: [2]

  • Nkhotakota - Kati
  • Nkhotakota - Kaskazini
  • Nkhotakota - Kaskazini Mashariki
  • Nkhotakota - Kusini
  • Nkhotakota - Kusini Mashariki

MarejeoEdit

  1. 2018 Population and Housing Census Main Report. Malawi National Statistical Office. Iliwekwa mnamo 25 December 2019.
  2. Parliament of Malawi - Members of Parliament - Nkhotakota District. Jalada kutoka ya awali juu ya 2016-06-02. Iliwekwa mnamo 2022-01-12.