Kano ni jimbo la kujitawala katika kaskazini ya Nigeria. Mji mkuu ni Kano.

Jimbo la Kano, Nigeria
Jimbo la Kano

Jimbo la Kano limepakana na majimbo ya Katsina, Jigawa, Kaduna na Bauchi. Jimbo lilianzishwa tar. 27 Mei 1967. Gavana wa kwanza alikuwa Abdu Bako kuanzia 1967 hadi Julai 1975. Ibrahim Shekarau amekuwa gavana tangu 29 Mei 2003.

Eneo la jimbo ni 20,131 km², idadi ya wakazi 10,077,638 (mwaka 2005). Msongamano wa watu hufikia wakazi 501 kwa kilimita ya mraba.

Jimbo lina maeneo ya utawala 44 ("Local Government Areas"). Haya ni: Ajingi, Albasu, Bagwai, Bebeji, Bichi, Bunkere, Dala, Dambatta, Dawakin-Kudu, Dawakin-Tofa, Doguwa, Fagge, Gabasawa, Garko, Garum-Mallam, Gaya, Gazewa, Gwale, Gwarzo, Kabo, Kano Municipal, Karaye, Kibiya, Kiru, Kumbotso, Kunchi, Kura, Madobi, Makoda, Minjibir, Nassarawa, Rano, Rimin-Gado, Rogo, Shanono, Sumaila, Takai, Tarauni, Tofa, Tsanyawa, Tudun-Wada, Ungongo, Warawa na Wudil.

Kano ni kitovu cha biashara na uzalishaji mali nchini. Asilimia ya umwagiliaji wa mashamba inazidi majimbo yote na kuruhusu kilimo mwaka wote.


 
Majimbo ya Nigeria
Abia | Abuja Federal Capital Territory | Adamawa | Akwa Ibom | Anambra | Bauchi | Bayelsa | Benue | Borno | Cross River | Delta | Ebonyi | Edo | Ekiti | Enugu | Gombe | Imo | Jigawa | Kaduna | Kano | Katsina | Kebbi | Kogi | Kwara | Lagos | Nasarawa | Niger | Ogun | Ondo | Osun | Oyo | Plateau | Rivers | Sokoto | Taraba | Yobe | Zamfara
Makala hii kuhusu maeneo ya Nigeria bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kano (jimbo) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.