Karen Hayes ni jina la uhusika wa kipindi cha televisheni cha Kimarekani maarufu kama 24. Uhusika unachezwa na Jayne Atkinson. Alianza kuonekana katika sehemu ya kumi na mbili ya msimu wa tano ya mfululizo na kupewa uhusika mkuu katika sehemu ya kumi na nane ya msimu wa sita.

Karen Hayes
muhusika wa 24

Jayne Atkinson kama Karen Hayes
Imechezwa na Jayne Atkinson
Mionekano
5, 6
Maelezo

Wazo na ushiriki hariri

Mwigizaji Laurie Metcalf ndiye aliyekuwa mwigizaji kamili wa uhusika huu wa Karen Hayes kabla kubadilishana na Jayne Atkinson.[1] Mtayarishaji Howard Gordon akathaminisha uwezo wa uigizaji wa Metcalf na kusema kwamba

uhusika haukuwa sahihi kwa mwigizaji huyu, hivyo wakambadilisha

Katika uhusika hariri

Kabla ya kujiunga na Jeshi la Usalama wa Taifa la Marekani, Hayes alikuwa kachero wa FBI. Alifanya katika kitengo cha kupambana na ugaidi cha FBI, na ikatokea kuwa Kachero Mkuu na kisha baadaye akawa Mkuu wa Kanda.

Hayes ana digrii ya mambo ya Sociology alioipata katika Chuo Kikuu cha Princeton.[2] Atkinson alidai kwamba, uhusika wake ni wa hatari hasa akiwa mitaani kwa raia wa kawaida huenda wakamzonga."[3]

Marejeo hariri

  1. "ROSEANNE - METCALF BOWS OUT OF 24". ContactMusic. 2005-12-19. Iliwekwa mnamo 2008-07-05. 
  2. "FOX 24- Character biography". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-02-12. Iliwekwa mnamo 2009-03-30. 
  3. Supporting players get to shine

Viungo vya Nje hariri