24 (msimu wa 5)
Msimu wa Tano (pia unajulikana kama Siku ya 5) ya mfululizo wa kipindi cha televisheni cha 24 kilichoanza kurushwa hewani kuanzia tar. 15 Januari 2006 na kumalizia msimu wake kunako tar. 22 Mei 2006.
Msimu wa 5 wa 24 | |
---|---|
Season 5 Cast | |
Nchi asilia | Marekani |
Mtandao | Fox Broadcasting Company |
Iko hewani tangu | 15 Januari 2006 – 22 Mei 2006 |
Idadi ya sehemu | 24 |
Tarehe ya kutolewa DVD | 5 Desemba 2006 |
Msimu uliopita | Msimu wa 4 |
Msimu ujao | Msimu wa 6 |
Hadithi ya Msimu wa Tano inaanza na kushia 7:00 asubuhi. Muda wake uko sawa na ule wa msimu uliopita.
Dakika 10 za mwanzo zilikuwa zikipatikana kwenye DVD ya msimu uliopita.[1] Ilikuwa ikirushwa kwenye Sky One huko nchini Uingereza kabla ya kuanza rasmi kwa msimu wa tano.
Muhtasari wa Msimu
haririMsimu wa Tano (2006) ni seti ya miezi 18 baada ya Msimu wa Nne.
Baada ya matukio ya Msimu wa Nne, kachero wa CTU Jack Bauer sasa hivi anafanyakazi siku-hadi-siku akiwa kama mfanyakazi wa kampuni ya kusafisha mafuta akiwa chini ya jina la "Frank Flynn" mjini Mojave, California. Jack arejea zake nyumbani huko mjini kaskazini mwa mji wa Los Angeles kwa Diane Huxley, mama asiye na mume, na mtoto wake mwenye umri miaka 15 aliyeitwa Derek.
Msimu wa Tano ilitakiwa iwe siku kubwa katika kipindi cha urais cha Charles Logan. Amepanga kusaini mkataba wa muungano kupinga ugaidi na Rais wa Urusi Bw. Yuri Suvarov kwa hiari yake huko mjini Hidden Valley, California. Hii ni siku ambayo inaaminika kwamba iliendeshwa kinyume sana kuliko matukio ya siku zote, kama Mrusi gaidi aliyejitenga na serikali yake (imekihiswa kuwa Chechen, ingawa hili halijaelezwa vizuri) ambaye yeye ndiye aliyebeba mzigo mzima wa mashambulizi kwa imani ya kuwa mkataba ule utaumiza watu zao.
Baadaye, ikagundulika kwamba yale matukio yaliyotokea ni sehemu kubwa sana ya njama za kiserikali ya rais alioko madarakani Bw. Rais Charles Logan, Mkubwa wa Wafanyakazi Walt Cummings, mkandarasi wa Kitengo cha Ulinzi Christopher Henderson, kwa ushirikiano wa James Nathanson, na kundi la watu ambao hawajulikani wanaongoza na kushawishi matendo ya Logan watokao katika sehemu zisizojulikana, wakiongozwa na mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la "Graham" ambaye inawezekana ndiye aliyefanya mpango wa Jack kujifichua kutoka mafichoni, na matukio yote.
Mpango wao wa awali ulikuwa kuachia gesi ya neva juu ya magaidi wa Kirusi na kutumia msamaha huo kama maombi ya kuachia vikosi vya kijeshi vya kupinga mkataba wa ugaidi, na kumruhusu Logan kulinda maslahi ya petroli ya Kimarekani huko Asia ya Kati. Rais wa zamani David Palmer alianza kulijua hili na akauawa ili kumnyamazisha; kifo chake kimekuwa mhamasiko mkubwa kwa harakati za Jack (mbali ya kusingiziwa kumwua David Palmer). Kama jinsi alivyoeleza kwa mara kadhaa kwenye mzunguko wa siku, "Haya mambo binafsi."
Njama kuu
haririNjama ndogo
haririWahusik wa Msimu
haririHii ni orodha ya washiriki wakuu wa Msimu wa 5. Tazama Orodha ya wahusika wa 24 kwa orodha iliyokamili.
Manyota
- Kiefer Sutherland kama Jack Bauer
- Kim Raver kama Audrey Raines
- Mary Lynn Rajskub kama Chloe O'Brian
- Carlos Bernard kama Tony Almeida
- Gregory Itzin kama Charles Logan
- James Morrison kama Bill Buchanan
- Roger Cross kama Curtis Manning
- Louis Lombardi kama Edgar Stiles
- Jean Smart kama First Lady Martha Logan
Special Guest Stars
- Elisha Cuthbert kama Kim Bauer
- Reiko Aylesworth kama Michelle Dessler
- William Devane kama Secretary of Defense James Heller
Wageni Maalumu Waliouza Sura
Wanaojirudia
- Sean Astin kama Lynn McGill
- Jude Ciccolella kama Mike Novick
- Julian Sands kama Vladimir Bierko
- Jayne Atkinson kama Karen Hayes
- Connie Britton kama Diane Huxley
- Brady Corbet kama Derek Huxley
- Geraint Wyn Davies kama James Nathanson
- Sandrine Holt kama Evelyn Martin
- Jonah Lotan as Spenser Wolff
- Paul McCrane kama Graem
- Glenn Morshower kama Aaron Pierce
- John Allen Nelson kama Walt Cummings
- Carlo Rota kama Morris O'Brian
- Mark Sheppard kama Ivan Erwich
- Stephen Spinella kama Miles Papazian
- Ray Wise kama Vice President Hal Gardner
- DB Woodside kama Wayne Palmer
- Peter Weller kama Christopher Henderson
Vifo
haririMsimu huu ni maarufu sana kwa idadi kubwa wahusika wakuu wanaouawa. Vifo vikubwa kabisa ni pamoja na cha David Palmer, Michelle Dessler, na Edgar Stiles. Tony Almeida aliuawa vilevile, ingawa kifo chake kilikuja kujulikana zaidi kwenye msimu wa saba. Wahusika wengine wadogo waliokufa ni pamoja na Walt Cummings na Lynn McGill. Aaron Pierce pia ilikuwa auawe, lakini Martha Logan aliona nini kilikuwa kinataka kutokea na kusaidia kuzuia lisitokee; kwa maana hiyo, Pierce ni muhusika pekee mwingine mbali na Jack Bauer kuonekana kwenye misimu yote saba ya mfululizo huu wa 24.[2]
Marejeo
hariri- ↑ Breaking News - ACTION-PACKED 10-MINUTE PREQUEL LEADS INTO NEW SEASON OF "24" | TheFutonCritic.com
- ↑ "TV week interview". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-02-14. Iliwekwa mnamo 2009-10-16.
Viungo vya Nje
hariri- Season 5 on 24 Wiki
- TV.com: 24 Season 5 Episode Guide Archived 19 Novemba 2009 at the Wayback Machine.
- Fox.com: Seasons 1-5 Episode Guides Archived 7 Machi 2009 at the Wayback Machine.