24 (msimu wa 6)
Msimu wa Sita (pia unajulikana kama Siku ya 6) ya mfululizo wa televisheni wa 24 ulioanza kurushwa hewani nchini Marekani mnamo siku ya Jumapili, 14 Januari 2007, Uingereza mnamo 21 Januari 2007 na nchini Australia mnamo 30 Januari 2007.
Msimu wa 6 wa 24 | |
---|---|
Season 6 Cast | |
Nchi asilia | Marekani |
Mtandao | Fox Broadcasting Company |
Iko hewani tangu | 14 Januari 2007 – 21 Mei 2007 |
Idadi ya sehemu | 24 |
Msimu uliopita | Msimu wa 5 |
Msimu ujao | Msimu wa 7 |
Hadithi ya msimu huu inaanza na kuisha saa 12:00 asubuhi. Ni seti ya miezi 20 baada ya matukio ya msimu wa tano.
Muhtasari wa msimu
haririMsimu wa Sita (2007) ni seti ya miezi 20 (Mei 2011) baada ya Msimu wa Tano. Wasanifu wa onyesho walieleza kwamba waliepuka matumizi ya tarehe ili kuacha mchezo "uende na wakati."[1]
Baada ya matukio ya Msimu wa Tano na zaidi ya majuma 11 ya kabla ya Siku ya 6, nchi ya Marekani ililengwa pwani-hadi-pwani na mfululizo wa wanaojiotoa mhanga na mabomu. Mtu mmoja aitwaye Abu Fayed amekubali kuwapa Marekani mahali pa gaidi Hamri Al-Assad, gadi anayedhaniwa kuwa ndiye muhusika mkuu wa mashambulizi hayo, kwa kubadilishana na kachero wa zamani wa CTU Jack Bauer ambaye alikuwa na ugomvi naye binafsi. Kwa kufuatia hilo, Rais Wayne Palmer akafanya mpango wa kutolewa kwa Bauer, ambaye alikamatwa kiharamu na Makachero wa Serikala ya China mwishoni mwa Siku ya 5, kwa makubaliano ya fedha nyingi mno.
Hata hivyo, wakati anapata mateso kutoka kwa Fayed, Bauer akagundua kwamba Assad ndiye hasa anayetaka kuzuia mashambulizi, na Fayed ndiye muhusika mkuu. Kwa bahati nzuri, Jack akaweza kutoroka, na kwenda kumwokoa Assad asije akauawa na shambulio la anga lililokuwa likitolewa na serikali yake. Jack na CTU, na msaada wa Assad, wakaweza kugundua nia ya kweli ya Fayed: kulipua bomu la nyuklia katika nchi ya Marekani. Baada ya shambulio moja la nyuklia, Jack ana kazi ya kutafuta uhueni wa mabomu ya nyuklia yaliyosalia, hivyo kupanga mfululizo wa matukio ya siku.
Wahusika
haririHii ni orodha ya wahusika wakuu wa Msimu wa 6. Tazama orodha ya wahusika wa 24 kwa orodha iliyokamilika kabisa.
Nyota
- Kiefer Sutherland kama Jack Bauer
- Mary Lynn Rajskub kama Chloe O'Brian
- DB Woodside kama Rais Wayne Palmer
- James Morrison kama Bill Buchanan
- Peter MacNicol kama Tom Lennox
- Jayne Atkinson kama Karen Hayes
- Carlo Rota kama Morris O'Brian
- Eric Balfour kama Milo Pressman
- Marisol Nichols kama Nadia Yassir
- Regina King kama Sandra Palmer
Nyota Waalikwa Wageni
- Kim Raver kama Audrey Raines
- William Devane kama James Heller
- Jean Smart kama Martha Logan
- Powers Boothe kama Vice President Noah Daniels
- Gregory Itzin kama Charles Logan
- James Cromwell kama Philip Bauer
Wanajirudia
- Roger Cross kama Curtis Manning
- Rena Sofer kama Marilyn Bauer
- Evan Ellingson kama Josh Bauer
- Nick Jameson kama Rais wa Urusi Yuri Suvarov
- Paul McCrane kama Graem Bauer
- Kari Matchett kama Lisa Miller
- Tzi Ma kama Cheng Zhi
- Rade Šerbedžija kama Dmitri Gredenko
- Adoni Maropis kama Abu Fayed
- Glenn Morshower kama Aaron Pierce
- Kathleen Gati kama Mke wa Rais Anya Suvarov
- Chad Lowe kama Reed Pollock
- Alexander Siddig kama Hamri Al-Assad
- Michael Shanks kama Mark Bishop
- Harry Lennix kama Walid Al-Rezani
- Kal Penn kama Ahmed Amar
- David Hunt kama Darren McCarthy
- Ricky Schroder kama Mike Doyle
Marejeo
hariri- ↑ Fienberg, Daniel (17 Januari 2007). "Looking for clues on the set of '24'". Zap2It.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-07-31. Iliwekwa mnamo 2009-07-31.
Viungo vy Nje
hariri- Season 6 on 24 Wiki
- TV.com: 24 Season 6 Episode Guide Ilihifadhiwa 25 Januari 2010 kwenye Wayback Machine.
- Fox.com: Seasons 1-6 Episode Guides Ilihifadhiwa 27 Aprili 2009 kwenye Wayback Machine.