Kasi (lat. & ing. Alkes, pia α Alfa Crateris, kifupi Alfa Crt, α Crt) ni nyota angavu ya pili katika kundinyota la Batiya (Crater).

Kasi (Alfa Crateris, Alkes)
Kasi (Alkes) katika kundinyota yake ya Batiya (Crater)
Kundinyota Batiya (Crater)
Mwangaza unaonekana 4.07[1]
Kundi la spektra K1 III
Paralaksi (mas) 20.49
Umbali (miakanuru) 159
Mwangaza halisi +0.44
Masi M☉ 1.81
Nusukipenyo R☉ 12.32
Mng’aro L☉ 66
Jotoridi usoni wa nyota (K) 4691
Majina mbadala 7 Crateris, NLTT 25942, LTT 4040, HD 95272, BD-17° 3273, HIP 53740, HR 4287, FK5 1283, SAO 156375.

Jina

Nyota ya Kasi ilijulikana kwa mabaharia Waswahili tangu miaka mingi wakifuata njia yao baharini wakati wa usiku kwa msaada wa nyota. [2]. Walipokea jina hili kutoka kwa Waarabu wanaosema الكأس al-ka’s inayomaanisha „bilauri, glasi" kwa kurejea umbo la kundinyota hii ndogo na dhaifu. Ptolemaio aliita "kwenye mguu wa bilauri" [3].

Kwa matumizi ya kimataifa Umoja wa Kimataifa wa Astronomia ulikubali jina la Kiarabu na kuorodhesha nyota hii kwa tahajia ya "Alkes" [4].

Alfa Crateris ni jina la Bayer ikiwa ni nyota angavu ya pili katika Batiya ingawa Alfa ni herufi ya kwanza katika Alfabeti ya Kigiriki.

Tabia

Kasi iko kwa umbali wa miakanuru takriban 160 kutoka Jua letu. Mwangaza unaoonekana ni mag 4.2.

Kasi ni nyota jitu jekundu inayoyeyunganisha heli kuwa kaboni na oksijeni katika kiini chake. Spektra yake inaonyesha mistari ya metali mbalimbali ambayo ni dokezo ya kwamba nyota hii ilianza maisha yake katika sehemu za ndani za Njia Nyeupe yaani galaksi yetu.[5]

Tanbihi

  1. Vipimo kufuatana na Reffert & alii (2015), kwa kutumia makadirio ya „horizontal branch“
  2. ling. Knappert 1993
  3. Tooner, Almagest (1984), uk 393
  4. Naming Stars, tovuti ya Umoja wa Kimataifa wa Astronomia (Ukia), iliangaliwa Novemba 2017
  5. taz. Kaler, Alkes

Viungo vya Nje


Marejeo

  • Allen, Richard Hinckley: Star-Names and their Meanings; kwa G. E. Stechert New York, Leipzig, London, Paris 1899, ukurasa 437 (online kwenye archive.org)
  • Knappert, Jan: The Swahili Names of Stars, Planets and Constellations; The Indian Ocean Review September 1993 Volume 6 No. 3 September 1993, kurasa 6-7, ISSN 1031-2331
  • Reffert, Sabine; Bergmann, Christoph; Quirrenbach, Andreas; Trifonov, Trifon; Künstler, Andreas (2015). "Precise radial velocities of giant stars. VII. Occurrence rate of giant extrasolar planets as a function of mass and metallicity". Astronomy & Astrophysics. 574: A116. online hapa