Kata (chombo)
Kwa kata kama ngazi ya ugatuzi tazama kata - Kwa maana nyingine tazama kata (maana)
Kata ni chombo maalumu kitumiwacho na makabila mengi nchini Tanzania, hasa na Wachagga huko Mkoa wa Kilimanjaro. Kata hutumika kunywea pombe iitwayo mbege.
Matengenezo
haririKata hutengenezwa kwa kutumia matunda ya jamii ya tikiti yaitwayo vibuyu. Matunda hayo hukatwa katikati, kisha hutolewa nyamanyama za ndani ili kupata uwazi ambao baada ya tunda kukaushwa hupatikana aina ya kikombe kizito kwa jina kibuyu. Kikombe hicho kikiisha kukauka hutobolewa kwa upana matundu mawili ambayo hukobekwa kijiti kirefu kitumikacho kama mshikio wa kata.
Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kata (chombo) kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |