Kebedech Tekleab
Kebedech Tekleab (kuzaliwa 1958) ni mchoraji, mchongaji wa sanamu na mshairi kutoka Ethiopia.
Tekleab alihudhuria shule ya sanaa iliyopo Addis Ababa alishiriki kwenye mapinduzi ya mwishoni mwa miaka ya 1970. Alikimbia Ethiopia, alishiriki kwenye vita ya nchi na Somalia, Alifungwa kwenye kambi ya kazi ngumu kwa muda uliokaribia muongo mmoja. Aliachiliwa huru mwaka 1989 na akaenda kuungana na familia yake iliyopo Marekani, alipata shahada ya sanaa mwaka 1992 na Shahada ya Uzamili mwaka 1995 kutoka chuo cha Howard. Alitoa kazi yake "Mfululizo wa Adhabu" kama sehemu ya tasnifu yake "Humanity In Descent: Visual Images Of Human Suffering".[1]
Tekleab amefundisha SCAD ambacho ni chuo cha Sanaa na Ubunifu kilichopo Savannah, Georgia na chuo cha Howard kilichopo jiji la New york. Hivi sasa anafundisha chuo cha Jiji la New York (The City University of New York) kilichopo New York.
Mwaka 2001, Tekleab alifanya kazi na Alexander Boghossian kwenye tamasha lililoitwa "Nexus" kwa ajikinya ukuta wa uwakilishi katika balozi ya Ethiopia iliyopo Washington D.C.[2] The work is an aluminum relief sculpture (365 x 1585 cm) mounted on the granite wall of the embassy.[2] Nexus inajumuisha mapambo ya motif, chati na alama kutoka mila za kidini za Ethiopia ikiwa ni pamoja na Ukristo, Uyahudi, Uislamu pamoja na mila zingne za kiasili, ikijumlisha hati zenye alama na fomu zinazowakilisha vyombo vya muziki vyombo vya matumizi na mimea na wanyama wa kikanda.[2]
Marejeo
hariri- ↑ Ellerson Poulenc, Beti (2008-06-17). "Words and Images of Kebedech Tekleab". Africultures. Iliwekwa mnamo 18 Aprili 2011.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 2.0 2.1 2.2 "Nexus". National Museum of African Art. 2003. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-06-06. Iliwekwa mnamo 16 Oktoba 2010.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kebedech Tekleab kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |