Kerrea Gilbert
Kerrea Kuche Gilbert (alizaliwa Hammersmith, London, 28 Februari 1987) alikuwa mchezaji wa kandanda wa Uingereza NA wa klabu ya Arsenal FC kama mlinzi.
Kerrea Gilbert | ||
Maelezo binafsi | ||
---|---|---|
Jina kamili | Kerrea Kuche Gilbert | |
Tarehe ya kuzaliwa | 28 Februari 1987 | |
Mahala pa kuzaliwa | Hammersmith,London, Uingereza | |
Urefu | 1.75m | |
Nafasi anayochezea | Difenda | |
Maelezo ya klabu | ||
Klabu ya sasa | Arsenal | |
Namba | 42 | |
Klabu za vijana | ||
2003–2005 | Arsenal FC | |
Klabu za ukubwani | ||
Miaka | Klabu | |
2005- 2006-2007 2007-2008 2008-2009 |
Arsenal Cardiff Southend United LeicesterCity | |
Timu ya taifa | ||
Uingereza | ||
* Magoli alioshinda |
Kazi
haririArsenal
haririGilbert alikuwa akicheza katika timu za vijana na timu hifadhi mpaka msimu wa 2005-06. Hata hivyo, baada ya majeruhi kwa wachezaji kadhaa katika timu ya Arsena ,Gilbert aliorodheshwa kama mchezaji mbadala wa difenda wengine. Alichezea timu ya kwanza kwa mara ya kwanza dhidi ya Reading katika Shindano la Kombe la League mnamo 29 Novemba 2005.Mnamo tarehe 7 Desemba alicheza katika mechi ya Ligi ya Mabingwa ya UEFA dhidi ya Ajax Amsterdam akiwa mchezaji mbadala kwa Lauren aliyekuwa ameumia.
Shida ya majeruhi katika timu ya Arsenal iliendelea ,ikampa nafasi ya kuanza mechi dhidi ya Cardiff City katika Shindano la Kombe la FA mnamo 7 Januari 2006.Alisifiwa kwa mbio zake za kasi na akacheza katika mechi sita baada ya mechi hiyo. Alicheza kwa mara ya kwanza katika Ligi Kuu ya Uingereza mnamo 21 Januari 2006 katika mechi dhidi ya Everton, walishindwa 1-0.Alicheza pia katika mikondo yote miwili ya nusu fainali ya Shindano la Kombe la League dhidi ya Wigan Athletic,alisaidia katika kufunga kwa bao la Thierry Henry.Arsenal walishindwa kwa shindano hilo.
Hata hivyo, Gilbert mwenyewe alipata majeraha katika mechi ya Arsenal na West Ham mnamo 1 Februari 2006,walishindwa 3-2.Alikatazwa kucheza kwa miezi miwili,hivyo basi ikamnyang'anya nafasi ya timu. Tangu Aprili 2006, amechezea timu ya Arsenal mara 9.
Cardiff City
haririTarehe 21 Julai 2006, Gilbert alihamia timu ya Cardiff City katika mpango wa mkopo katika msimu wa 2006-07. Gilbert alianza msimu katika klabu hiyo kama difenda wa upande wa kulia na akacheza mara kwa mara katika timu hiyo hadi Desemba. Hata hivyo,alipata majeraha madogo yaliyomfanya asicheze mechi kadhaa. Nafasi yake ilichukuliwa na Chris Gunter na hakuweza kumtoa Chris hapo na hakucheza sana katika mechi zilizobaki katika msimu huo. Gilbert akacheza mechi 26 katika timu hiyo ya Cardiff.
Southend United
haririYeye alijiunga na Southend United kwenye mpango wa mkopo wa miezi sita mnamo tarehe 30 Julai 2007. [5] Alicheza mechi sita katika timu hiyo ya Southend kabla ya kutopendwa na meneja Steve Tilson na kutohusishwa katika timu. Yeye alirudi timu ya Arsenal mnamo tarehe 3 Januari 2008. [7]
Kurudi Arsenal
haririBaada ya kurudi timu ya Arsenal, Gilbert alipewa jezi ya # 46 na akaorodheshwa kama mchezaji mbadala katika mechi ya ligi dhidi ya Blackburn mnamo 11 Februari 2008,hakucheza mechi hiyo.
Leicester City
haririTarehe 10 Julai 2008, Gilbert alijiunga na Leicester City katika mpango wa mkopo wa msimu mzima wa 2008-2009. Yeye alifunga bao lake la kwanza ya ligi yake katika mechi dhidi ya Stockport County iliyoisha 1-1.
Kurudi Arsenal
haririKatika msimu wa 2009-10, Gilbert alirejea Arsenal. Yeye alicheza katika mechi ya Arsenal dhidi ya West Bromwich Albion katika Shindano la Kombe la League,akicheza dakika zote 90 huku wakishinda 1-0. Kerrea ,pia, alicheza katika Shindano la Kombe la League waliposhinda Liverpool 2-1. Alishiriki katika mechi yake ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa baada ya miaka minne,dhidi ya Olympiakos.Timu iliyocheza siku hiyo ilikuwa timu kijana kabisa kucheza katika shindano hilo ikiwa na umri wa miaka 21,hii ilivunja rekodi ya hapo awali iliyoshikiliwa na Ajax.
Takwimu ya Wasifu
hariri- (sahihi tangu 9 Desemba 2009)
Klabu | Msimu | Ligi | Mashindano ya kombe yote | Uropa(Ligi ya Mabingwa ya UEFA) | Total | ||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Mechi alizocheza | Mabao | Mechi alizocheza | Mabao | Mechi alizocheza | Mabao | Mechi alizocheza | Mabao | ||
Arsenal | 2005–06 | 2 | 0 | 6 | 0 | 1 | 0 | 9 | 0 |
2006–07 | Msimu aliokuwa katika mpango wa mkopo | ||||||||
2007–08 | Msimu aliokuwa katika mpango wa mkopo | ||||||||
2008–09 | Msimu aliokuwa katika mpango wa mkopo | ||||||||
2009–10 | 0 | 0 | 2 | 0 | 1 | 0 | 3 | 0 | |
Cardiff City | 2006–07 | 24 | 0 | 2 | 0 | - | 26 | 0 | |
Southend United | 2007–08 | 5 | 0 | 1 | 0 | - | 6 | 0 | |
Leicester City | 2008–09 | 34 | 1 | 5 | 0 | - | 39 | 1 | |
Jumla | 2005– | 65 | 1 | 16 | 0 | 2 | 0 | 83 | 1 |
*KUMBUKA timu katika Kiitaliki inaonyesha msimu aliokuwa katika mpango wa mkopo in
Tuzo
hariri- Leicester City
- Ligi ya Kwanza ya Uingereza : 2008–09
Marejeo
hariri- BBC Sport. 2006-07-21. "Cardiff sign Glombard and Gilbert"
- BBC Sport. 2007-07-30. "Arsenal's Gilbert joins Southend".
- Yahoo! Sports. 2008-01-03. "Shrimpers bid Gilbert farewell".
- BBC Sport. 2008-07-10. "Leicester sign Arsenal's Gilbert".
- "Leicester 1-1 Stockport". BBC. 3 Machi 2009. "Leicester 1-1 Stockport".
Viungo vya nje
hariri- Kerrea Gilbert career stats kwenye Soccerbase
- arsenal.com Ilihifadhiwa 2 Julai 2009 kwenye Wayback Machine.