Kimandarini
Kimandarini ni lugha ya Kisino-Tibeti nchini Uchina inayozungumzwa na Wachina. Mwaka wa 2000 idadi ya wasemaji wa Kimandarini nchini Uchina imehesabiwa kuwa watu milioni 840. Pia kuna wasemaji katika nchi zifuatazo: 24,320,000 nchini Taiwan (1993), 10,600 nchini Brunei (2006), 60,900 ndani ya Hong Kong (2006), 460,000 nchini Indonesia (1982), wengi nchini Malaysia ambapo ni lugha ya taifa (lakini bila idadi rasmi ya wasemaji), 35,000 nchini Mongolia (1993), 500,000 nchini Myanmar (1994), 500 nchini Ufilipino (1990), 1,210,000 nchini Singapuri (2010), na 5,880 nchini Uthai (1984). Kufuatana na uainishaji wa lugha, Kimandarini iko katika kundi la Kichina.
Sauti na toni
haririTabia ya pekee ya lugha za Kichina ni tofauti kubwa kati ya toni za sauti. Silabi "ma" inaweza kuwa na maana 4 tofauti kabisa kufuatana na matamshi tofauti ya toni.
Toni ya 1 | Toni ya 2 | Toni ya 3 | Toni ya 4 |
---|---|---|---|
toni ileile ya juu | toni yapanda juu | toni yashuka na kupanda juu |
toni ya kushuka vikali |
mā=mama | má=bangi | mǎ=farasi | mà=kutukana |
Uenezi
haririKimandarini ni lugha rasmi katika Jamhuri ya Watu wa China, Jamhuri ya China (Taiwan) na Singapuri. Husemwa pia na raia Wachina katika Indonesia na Malaysia.
Viungo vya nje
hariri- lugha ya Kimandarini kwenye Multitree
- makala za OLAC kuhusu Kimandarini Ilihifadhiwa 11 Agosti 2015 kwenye Wayback Machine.
- lugha ya Kimandarin katika Glottolog
- lugha ya Kimandarini kwenye Ethnologue
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kimandarini kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |