Kieran Gibbs

Wachezaji mpira wa Uingereza
Kieran Gibbs
Maelezo binafsi
Jina kamili James Ricardo Kieran Gibbs
Tarehe ya kuzaliwa 26 Septemba 1989
Mahala pa kuzaliwa    Lambeth, London, Uingereza
Urefu m 1.80 (5 ft 11 in)
Nafasi anayochezea Difenda
Maelezo ya klabu
Klabu ya sasa Arsenal
Namba 28
Klabu za vijana
2001–2004
2004–2007
Wimbledon
Arsenal
Klabu za ukubwani
Miaka Klabu
2007–2017 Arsenal
Norwich City (mpango wa mkopo)
Timu ya taifa
2007–2009 Uingereza

* Magoli alioshinda

Historia

hariri

James Ricardo Kieran Gibbs (alizaliwa 26 Septemba 1989) ni mchezaji wa kandanda wa Uingereza ambaye huchezea timu ya Arsenal kama mchezaji wa nyuma. Yeye alihudhuria Shule ya Upili ya Riddlesdown katika eneo la Purley,Kusini mwa London.

Wasifu

hariri

Wasifu wa Klabu

hariri

Gibbs alianza kazi yake katika shule ya Wimbledon lakini akahamia Arsenal ,pamoja na Abu Ogogo na James Dunne, Wimbledon ilipoachishwa kazi katika mwaka wa 2004 na ikawa Milton Keynes Dons. Yeye alicheza katika nafasi ya kati na pia kwenye upande wa kushoto. Yeye alihusika mara kwa mara katika timu ya Arsenal ya vijana walio chini ya umri wa miaka 18 na timu hifadhi.Alicheza pia mechi za kirafiki dhidi ya Barnet na Inter Milan. Mnamo Septemba 2007, Gibbs alitia saini mkataba na Arsenal, na alikuwa mmojawapo katika timu iliyotajwa kucheza katika msimu wa 2007-08 Ligi ya Mabingwa ya UEFA na akapewa jezi nambari 34.

Yeye alichezea timu rasmi ya Arsenal kwa mara ya kwanza alipoashiriki katika mechi ya Shindano la Kombe la League dhidi ya Sheffield United mnamo 31 Ktoba 2007.Alicheza tena ,kwa mara ya pili, alipoingia kama mchezaji mbadala wa Eduardo da Silva katika robo fainali dhidi ya Blackburn Rovers,18 Desemba 2007.

Tarehe 31 Januari 2008, yeye alikubali mpango wa mkopo ambao angeenda kucheza katika timu ya Norwich City hadi mwisho wa msimu wa 20007-08. Yeye alirudi Arsenal mwanzoni mwa mwezi wa 29 Aprili 2008 na akachukua nafasi yake katika timu hifadhi ya Arsenal> Yeye alikwenda na kuchaguliwa kama mchezaji mbadala wa kuingia kucheza katika mechi dhidi ya Everton mnamo 4 Mei 2008 lakini hakucheza.

Alicheza katika mechi za kabla ya msimu wa 2008-09,mara nyingi akicheza kama difenda kule nyuma, na akawa mchezaji ambaye hakutumiwa katika mechi dhidi ya Fulham walioshindwa 1-0,24 Agosti 2008, na pia hakutumiwa katika ushindi wao dhidi ya Bolton Wanderers wa 3-1(Septemba). Gibbs aliendelea kucheza katika Shindano la Kombe la League na akacheza dakika 90 katika ushindi wa 6-0 dhidi ya Sheffield United katika raundi ya tatu ya mechi,23 Septemba 2008. Yeye,pia, alicheza waliposhinda 3-0 dhidi ya Wigan Athletic na vilevile alicheza katika mechi ya kushindwa dhidi ya Burnley katika hatua ya robo fainali. [14] [15] [16] Yeye alicheza kwa mara ya kwanza katika Shindano la Ligi ya Mabingwa ya UEFA mnamo 10 Desemba 2008 dhidi ya Porto FC akiwa mchezaji mbadala wa Abou Diaby.

Gibbs alicheza kwa mara ya kwanza katika Ligi Kuu Ya Uingereza dhidi ya Tottenham Hotspurs mnamo 8 Februari 2009 akiingia kama mchezaji mbadala wa Gael Clichy aliyeumia katika mechi hiyo.

 
Gibbs katika mazoezi

Clichy akiwa ameumia, Gibbs alianza mechi yake ya kwanza katika Ligi ya Mabingwa katika robo fainali dhidi ya Villareal mnamo 15 Aprili 2009,Arsenal ilishinda 3-0. Gibbs alianza kucheza mechi ya Shindano la Kombe la FA dhidi ya Chelsea na akamsaidia Theo Walcott kufunga bao. Alihusika ,pia, wakati Arsenal na Liverpool walipotoka sare dhidi ya Liverpool, 21 Aprili, huko Anfield.Aliokoa timu yake kwa kupiga mpira ulipokuwa karibu kuingia goli.

Baada ya kucheza mechi mingi katika timu rasmi kwa kuwa Clichy alikuwa ameumia, Gibbs alicheza katika nusu fainali ya Shindano ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Manchester United,Arsenal walishindwa 1-0. Hata hivyo, katika mkondo wa pili wa mnusu fainali hiyo, Gibbs alifanya kosa lililomwezesha Park Ji-Sung kufunga bao muhimu sana baada ya dakika 7. [21]

Alianza katika mchuano wa kwanza wa Arsenal wa ufunguzi wa msimu dhidi ya Portsmouth na akacheza dakika 90. Clichy alipojeruhiwa na kutoweza kucheza kwa wiki kadhaa,Arsene Wenger alimpa Gibbs nafasi katika timu. Hata hivyo,mnamo tarehe 24 Novemba, Gibbs alivunjika mfupa mguuni katika mechi dhidi ya Standard Liege na jeraha hili likamtoaa kwa mchezo kwa wakati usiojulikana,Arsenal ilishinda 2-0.

Wasifu wa Kimataifa

hariri

Yeye alikuwa katika timu ya Uingereza ya vijana wa chini ya umri wa miaka 19 ambayo ilishindwa katika mkondo wa vikundi katika Shindano la UEFA la 2008 la vijana wa chini ya umri wa miaka 19.Hata hivyo, walihitimu kucheza katika Shindano la Kombe la Dunia la vijana wa chini ya umri wa miaka 20 nchini Misri lililoandaliwa na FIFA.

Gibbs aliitwa kujiunga na kikosi cha Uingereza cha vijana wa chini ya umri wa miaka 21 akiwa pamoja na mwenzake kutoka Arsenal ,Theo Walcott.Walichaguliwa ili wacheza katika shndano la Uropa la 2009 la vijana wa chini ya umri wa miaka 21 nchin Uswidi. Yeye alifunga mabao mawili katika mchuano wa kirafiki na Azerbaijan kabla ya shindano mnamo 8 Juni 2009,walishinda 7-0.Alifunga mkwaju wake wa penalti katika nusu fainali ya shindano hilo dhidi ya Uswidi.

Stuart Pearce alimworodhesha Gibbs katika mechi za kuhitimu kucheza katika shindano la Mabingwa wa Uropa ya 2011. Yeye alifunga bao la kwanza katika ushindi wao wa 6-3 dhidi ya Masedonia hapo 9 Oktoba.

Takwimu ya Wasifu

hariri
(sahihi 24 Novemba 2009)
Klabu Msimu Ligi Kombe la FA Kombe la League Uropa Jumla
Mechi alizocheza Mabao Usaidizi wa kufunga bao Mechi alizocheza Mabao Usaidizi wa kufunga bao Mechi alizocheza Mabao Usaidizi wa kufunga bao Mechi alizocheza Mabao Usaidizi wa kufunga bao Mechi alizocheza Mabao Usaidizi wa kufunga bao
Arsenal 2007–08 0 0 0 0 0 0 2 0 1 0 0 0 2 0 1
Norwich City (mpango wa aina ya mkopo) 2007–08 7 0 0 0 0 0 0 0 0 0 0 0 7 0 0
Arsenal 2008-09 8 0 0 6 0 1 3 0 1 4 0 0 21 0 2
Arsenal 2009-10 3 0 0 0 0 0 2 0 0 2 0 1 7 0 1
Jumla 18 0 0 6 0 1 7 0 2 6 0 1 37 0 4

Arsenal FC

hariri

IKimataifa

hariri
  • Nafasi ya pili katika Shindano la Mabingwa ya UEFA kwa vijana walio chini ya umri wa 21(2009)


Binafsi

hariri

Marejeo

hariri
  1. Gibbs and Dunne delighted by pro contract, Ilihifadhiwa 26 Machi 2009 kwenye Wayback Machine. arsenal.com,
  2. "2007/08 UEFA Champions League - Matchweek Stats Pack". UEFA. http://www.uefa.com/printoutfiles/competitions/ucl/2008/e/e_01_md.pdf.
  3. "Sheff Utd 0-3 Arsenal". BBC Sport. 2007-10-31. http://news.bbc.co.uk/sport2/hi/football/league_cup/7065196.stm..
  4. Blackburn 2-3 Arsenal (aet), bbc.co.uk,
  5. Sky Sports | Football | Premier League | Arsenal | Canaries swoop for Gibbs
  6. Reserves: Aston Villa v Arsenal - Preview Ilihifadhiwa 30 Aprili 2008 kwenye Wayback Machine.
  7. Arsenal.com Ilihifadhiwa 12 Mei 2008 kwenye Wayback Machine.
  8. "Fulham 1-0 Arsenal". Arsenal.com. http://www.arsenal.com/match-menu/3003005/first-team/fulham-v-arsenal?tab=report Ilihifadhiwa 26 Agosti 2008 kwenye Wayback Machine..
  9. Arsenal 6-0 Sheff Utd, BBC Sport,
  10. Arsenal 3-0 Wigan , BBC Sport,
  11. Burnley 0-2 Arsenal , BBC Sport,

Viungo vya nje

hariri