Lugha za Kirumi

Lugha za Kirumi ni lugha zilizotokana na Kilatini kilichokuwa moja kati ya lugha za kale za Kihindi-Kiulaya.

Lugha za Kirumi duniani:
buluuKifaransa; kijaniKihispania; machungwaKireno; njanoKiitalia; nyekunduKiromania

Ni lugha mama kwa watu milioni 800 hivi duniani.

Zimehesabiwa hadi lugha 23 za namna hiyo, ingawa baadhi kwa wengine ni lahaja tu. Tena kuna Krioli nyingi zenye asili katika lugha hizo. Kati ya Krioli hizo, ile ya Haiti na ile ya Shelisheli ni lugha rasmi nchini.

Kilatini cha Roma ya Kale kama lugha mamaEdit

Kilatini kilikuwa lugha rasmi ya utawala, elimu na biashara ya Dola la Roma lililotawala maeneo ya Ulaya ya Kusini, Ulaya ya Magharibi, Afrika ya Kaskazini na Asia ya Magharibi kwa miaka mingi, hasa kati ya karne ya 1 KK na karne ya 5 BK.

Kilatini kiliendelea kuwa lugha ya watu wengi katika maeneo mbalimbali ya himaya hii kubwa hasa mijini.

Katika sehemu hizo zilijitokeza lahaja za pekee kulingana na lugha asilia za wenyeji.

Baada ya kuporomoka kwa Dola la Roma la Magharibi, lahaja hizo za Kilatini katika nchi mbalimbali ziliendelea kuchanganyikana na lugha hizo na zile za makabila ya Wagermanik yaliyoteka maeneo hayo yote na hatimaye zikawa lugha za pekee.

Lugha za Kirumi zinazotumiwa kitaifa:Edit

Lugha ambazo ni muhimi zaidi kama lugha za kitaifa ni:

Lugha za Kirumi zinazotumiwa kieneo:Edit

Lugha za kimataifaEdit

Lugha za Kihispania, Kifaransa na Kireno zimesambaa duniani kwa sababu ni lugha kuu za nchi ambazo zilikuwa na makoloni mengi, zikaacha lugha zao katika nchi nyingi, hasa Kihispania ambacho ni lugha kuu ya bara la Amerika, Kireno ambacho ni lugha rasmi ya Brazili na nchi 5 za Afrika na Kifaransa ambacho ni lugha rasmi katika nchi nyingi za Afrika, Amerika visiwani na Kanada.

Kiitalia ni mojawapo ya lugha rasmi za Uswisi, pamoja na nchi ndogondogo za San Marino na Vatikani.

Kiromania ni lugha rasmi ya Moldova pia, ingawa kwa jina la lahaja yake ya Kimoldova.

TanbihiEdit

 • (1988) The Romance Languages. London: Routledge. 
 • Posner, Rebecca (1996). The Romance Languages. Cambridge: Cambridge University Press. 
 • (2010) Romance Languages: A Historical Introduction. Cambridge: Cambridge University Press. 

Mabadiliko

 • Boyd-Bowman, Peter (1980). From Latin to Romance in Sound Charts. Washington, D.C.: Georgetown University Press. 

Misamiati

 • (1988) Lexikon der Romanistischen Linguistik. (LRL, 12 volumes). Tübingen: Niemeyer. 

Kifaransa

Kireno

 • Williams, Edwin B. (1968). From Latin to Portuguese, Historical Phonology and Morphology of the Portuguese Language, 2nd, University of Pennsylvania. 

Kihispania

 • Penny, Ralph (2002). A History of the Spanish Language, 2nd, Cambridge: Cambridge University Press. 
 • Lapesa, Rafael (1981). Historia de la Lengua Española. Madrid: Editorial Gredos. 
 • Vicente, Alonso Zamora (1967). Dialectología Española, 2nd, Madrid: Editorial Gredos. 

Kiitalia

 • (2002) I Dialetti delle Regioni d'Italia, 3rd, Milano: RCS Libri (Tascabili Bompiani). 
 • (1999) Il Linguaggio d'Italia. Milano: RCS Libri (Biblioteca Universale Rizzoli). 

Viungo vya njeEdit

  Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Lugha za Kirumi kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.