Kiev (pia:Kyiv - Kiukraine: Київ) ni mji mkuu wa Ukraine na pia mji mkubwa wa nchi hii wenye wakazi milioni mbili. Iko kando la mto Dnepr kwa 50°27′00″N, 30°31′24″E.

Mahali pa Kiev nchini Ukraine

Historia

hariri

Kiev inaaminiwa iliundwa mnamo ya karne ya 6 BK. Iliendelea kuwa mji mkuu wa Rus iliyokuwa milki kubwa ya kwanza ya Waslavoni ya mashariki. Mtemi Mkuu Vladimir I aliamua kupokea Ukristo akaamuru wakazi wote kubatizwa mtoni mara moja. Katika kumbukumbu la Ukraine na Urusi hii ilikuwa chanzo cha utamaduni wa kiorthodoksi wa Waslavoni ya mashariki. Hivyo Kiev inaitwa "mji mama wa miji yote ya Urusi".

Tar. 6 Desemba 1240 Kiev ilitekwa na jeshi la Wamongolia na kuchomwa moto. Mji ukafufuka tena lakini ukaendelea kuwa mji mdogo na makao makuu ya jimbo la Ukraine chini ya nchi mbalimbali zilizotawala yehemu hiyo kama Poland au Urusi.

Kiev ikaanza kukua na kuwa mji mkubwa wa tatu wa Milki ya Urusi katika mapinduzi ya viwandani ya karne ya 19. Baada ya mapinduzi ya Kibolsheviki ikawa mji mkuu wa Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kiukraine ndani ya Umoja wa Kisovyeti. Kiev iliharibiwa vibaya wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia ikajengwa upya na kukua. Ajali ya kinyuklia ya Chernobyl ilitokeea karibu na mji lakini haikuuathiri sana kwa sababu upepo ulipeleka mavumbi ya sumu upande mwingine. Tangu uhuru wa Ukraine mwaka 1991 mji mkuu wa nchi hii.

Picha za Kiev

hariri
  Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kiev kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.