Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kiukraine

Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kiukraine ilikuwa kati ya jamhuri wanachama 15 za Umoja wa Kisovyeti hadi mwaka 1991.

Bendera ya Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Ukraine.
Nembo yake.

Jina lake liliandikwa kwa alfabeti ya Kikirili katika lugha ya Kiukraine: "Українська Радянська Соціалістична Республіка, УРСР" (Ukrainska Radyanska Sotsialistichna Respublika, URSR) na pia kwa Kirusi "Украинская Советская Социалистическая Республика" (Ukrainskaya Sovyetskaya Sotsialisticheskaya Respublika, USSR).

Mji mkuu wa kwanza ulikuwa Kharkiv lakini serikali ilihamia Kiev mwaka 1934.

Jamhuri hii ilikuwa moja ya nchi wanachama walioanzisha Umoja wa Mataifa.[1] Hali halisi haikuwa na madaraka ya pekee kwa sababu ilikuwa chini ya usimamizi wa serikali kuu ya Moscow.

Baada ya kuporomoka kwa Umoja wa Kisovyeti nchi ilipata uhuru wake na kuwa nchi Jamhuri ya Ukraine.

Marejeo hariri

Coordinates: 50°27′N 30°30′E / 50.450°N 30.500°E / 50.450; 30.500