Kifungambuzi
Kishungi cha kifungambuzi
Kishungi cha kifungambuzi
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Plantae (Mimea)
(bila tabaka): Angiospermae (Mimea inayotoa maua)
(bila tabaka): Monocots (Mimea ambayo mche wao una jani moja)
(bila tabaka): Commelinids (Mimea kama jaja)
Oda: Poales (Mimea kama manyasi)
Familia: Poaceae (Manyasi)
Nusufamilia: Chloridoideae
Jenasi: Eleusine
Spishi: E. indica
(L.) Gaertn.

Kifungambuzi (Eleusine indica) ni spishi ya nyasi katika nusufamilia Chloridoideae. Asili kamili ya nyasi hili haijulikani kwa uhakika lakini yumkini linatoka Afrika au labda Asia. Siku hizi linatokea mahali popote kwa kanda za tropiki na nusutropiki. Spishi hii ni gugu baya shambani na imeanza kupinga viuamimea, kama glyphosate. Wanyama wafugwao hula nyasi hili lakini wakila mingi wanaweza kuugua kwa sababu ya sumu ndani ya majani (glycosides).

Kuna uwezekano mkubwa kama E. indica imezaa E. coracana au mwimbi kwa kuongeza maradufu nambari ya chembeuzi. Kwa hivyo mwimbi ni tetraploidi. Hata punje za kifungambuzi zinaweza kuliwa na hutumika pengine wakati wa uhaba wa chakula.

Viungo vya nje hariri

Picha hariri