Kijogoo-shamba

Ndege wa familia Calyptomenidae
Kijogoo-shamba
Kijogoo-shamba utosi-mweusi
Kijogoo-shamba utosi-mweusi
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Passeriformes (Ndege kama shomoro)
Familia ya juu: Eurylaimoidea (Ndege kama vijogoo-shamba)
Familia: Calyptomenidae (Ndege walio na mnasaba na vijogoo-shamba)
Ngazi za chini

Jenasi 2, spishi 6 + 1 kutoka familia nyingine:


Vijogoo-shamba au bandabanda ni ndege wa familia Calyptomenidae. Zamani ndege hawa waliainishwa katika familia Eurylaimidae lakini siku hizi inabaki spishi moja tu ndani yake, kijogoo-shamba kijani.

Wana domo pana na spishi za Asia pamoja na kijogoo-shamba kijani zina rangi ya majani lakini spishi nyingine za Afrika ni kahawia na nyeupe zenye michirizi myeusi. Ndege hawa wanatokea misitu mizito. Hula matunda na hukamata wadudu kwa namna ya shore au chechele. Hupenda kuwa kwa makundi ya hadi kufikia ndege 20. Tago la vijogoo-shamba ni mjengo mkubwa (mpaka nusu mita) unaofungika na wenye mwingilio kwa upande wake. Limefumika kwa vitawi, manyasi na majani na kufunikika kwa tando za buibui, vigoga na kuvumwani. Jike huyataga mayai 1-3.

Spishi za Afrika

hariri

Spishi za Asia

hariri