Kiki Gyan (anayejulikana pia kama Kiki Djan; 7 Juni 1957 - 10 Juni 2004) alikuwa mwanamuziki wa Ghana. Alikuwa mpiga kinanda wa bendi ya Osibisa ambayo ilikuwa maarufu miaka ya 1970. Pia alirekodi na kutoa albamu ya nyimbo za disco. Alikuwa na uwezo mkubwa ambaye angeweza kucheza kibodi vizuri sana.[1][2][3]

Maisha ya awali

hariri

Alizaliwa katika familia ya tabaka la kati huko Takoradi, Ghana.[4] Gyan alianza kucheza piano akiwa na umri wa miaka mitano na akaanza kufanya kazi ya kitaalam akiwa na miaka 12.[5] Aliacha shule ya upili akiwa na miaka 14 na baada ya ziara yake London na bendi ya wenyeji ya Ghana inayoitwa Pagadija;[4] alijiunga na kikundi cha Afro-rock cha Osibisa cha Uingereza baada ya talanta yake kutambuliwa na kaka wa mwanzilishi wa bendi hiyo.[6] Alikuwa na umri wa miaka 15 tu alipoanza kucheza na Osibisa mnamo 1972, akichukua nafasi ya mpiga kinanda ambaye alikuwa ameondoka tu, na alisafiri kimataifa na bendi wakati wa miaka ya 1970, akiitumbuiza hadhira kubwa ulimwenguni.[6]

Marejeo

hariri
  1. "Kiki Gyan". Discogs (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-08-11.
  2. Hakeem (2019-11-07). "An Introduction to Kiki Gyan's Magical Moments". DANDANO (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-08-11.
  3. "Sad: Do You Know Talented And Rich Kiki Gyan Of Osibisa Fame? His Life And How He Died Sorrowfully - Opera News". gh.opera.news. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-08-11. Iliwekwa mnamo 2021-08-11.
  4. 4.0 4.1 Riches to rags: Ghana mourns music hero (kwa Kiingereza (Uingereza)), 2004-06-10, iliwekwa mnamo 2021-08-11
  5. "Say No to Drugs - Kiki Djan". Modern Ghana (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-08-11.
  6. 6.0 6.1 "The Sad Story Of Sensational Keyboardist ?Kiki Gyan?". GhanaWeb (kwa Kiingereza). -001-11-30T00:00:00+00:00. Iliwekwa mnamo 2021-08-11. {{cite web}}: Check date values in: |date= (help)