Kikisi-Kaskazini ni lugha ya Kiniger-Kongo nchini Guinea na Sierra Leone inayozungumzwa na Wakissi. Lugha nyingine ya Kikisi ni Kikisi-Kusini nchini Liberia. Lugha hizo mbili zisichanganywe na lugha ya Kikisi nchini Tanzania. Mwaka wa 1991 idadi ya wasemaji wa Kikisi-Kusini nchini Guinea imehesabiwa kuwa watu 287,000. Pia kuna wasemaji 40,000 nchini Sierra Leone. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kikisi-Kaskazini iko katika kundi la Kiatlantiki.

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kikisi-Kaskazini kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.