Kingasa
Kingasa (au Kiongamo) ni lugha ya Kinilo-Sahara nchini Tanzania inayozungumzwa na Wangasa. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kingasa kiko katika kundi la Kinilotiki.
Mwaka wa 1983 idadi ya wasemaji wa Kingasa imehesabiwa kuwa watu 200 tu, yaani lugha imekaribia kutoweka kabisa. Ingawa kulikuwa na Wangasa zaidi ya 4,000 mwaka wa 2000, wengi walikuwa wameshasahau lugha yao na kutumia Kimaa, Kichaga au lugha nyinginezo. Inawezekana kwa sasa hakuna anayejua tena Kingasa.
Viungo vya nje
hariri- lugha ya Kingasa kwenye Multitree
- makala za OLAC kuhusu Kingasa Archived 19 Mei 2015 at the Wayback Machine.
- lugha ya Kingasa katika Glottolog
- http://www.ethnologue.com/language/nsg
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kingasa kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |