Kinilamba (au Kinyiramba, pamoja na lahaja ya Kiiambi) ni lugha ya Kibantu nchini Tanzania inayozungumzwa na Wanilamba. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kinilamba iko katika kundi la F30.

Mwaka wa 2006 idadi ya wasemaji wa Kinilamba imehesabiwa kuwa watu 455,000, ambao 50,000 ni Waiambi.

Kinyiramba asili yake ni Kibantu. Ushahidi wa kiisimu ni ushahidi unaothibitishwa kwa misingi inayohusu Sayansi ya Lugha.

1. Tungo (Sentensi) za Kinyiramba Miundo ya tungo (sentensi) za maneno ya Kinyiramba zinafanana sana na miundo ya tungo za maneno ya Kibantu. Kwani sentensi za Kinyiramba na lugha za Kibantu zina kiima na kiarifu. K A Mfano: Kinyiramba - Baba / Ulyea Ugali Kiswahili - Baba / anakula ugali

2. Vitenzi vya Kinyiramba na Kibantu Kuna uhusiano mkubwa sana kati ya vitenzi vya Kinyiramba na vile vya Kibantu (a) Viambishi Lugha ya Kinyiramba na lugha za kibantu vitenzi vyake hujengwa na mzizi (kiini) pamoja na Viambishi vyake (awali na tamati) Mfano :- Kinyiramba - u – Lim – a Kiswahili - a –na- lim-a - Lim – ni mzizi/ kiini - A – kiambishi tamati (b) Mnyambuliko wa kitenzi Mnyambuliko wa vitenzi vya kinyiramba hufanana na ule wa vitenzi vya lugha ya kibantu. Mfano: Kinyiramba - Kusheka - Kushekesha – Kushekolela Kiswahili - Kucheka – kuchekesha – Kuchekeea (c) Mwanzo wa Vitenzi Vitenzi vyote vya Kinyiramba na vile vya lugha za Kibantu huanza na viambishi viwakilishi nafsi. Mfano: Kinyiramba - Nigenda - Nalongola Kiswahili - Ninatembea - Nakwenda Kiambishi Ni, Na ni viambishi viwakilishi nafsi. (d) Mwishilizo wa vitenzi Vitenzi vya lugha za Kibantu na Kiswahili huishia na Irambu – a Mfano: Kinyiramba - Kukisiga Kua Manka Kiswahili - Kucheza Piga Kimbia

Lugha ya Kinyiramba hutumia lugha ya picha ambao huwa ya ukweli na maana ya uficho sana ambapo huweza kufisha ujumbe kwa jamii ili kujifunza. Mfano, Semi za Kinyiramba: - NA KINYIRAMBA KISWAHILI KIIUNGEREZA 1 Mwili kisonga Mukola Mwili hutunzwa na mwenyewe The body is kept by owne 2 Inkamilo zikilonda Undugu ni Kushirikiana Fraternity/Brotherhood is cooperation 3 Intondo imalunde Ipo siku moja One day yes 4 Nishunta intondo lukapinda Nasogeza siku kadri Mungu anavyonijalia I buy a day by providence 5 Nukuduma ukuligagya Atafutaye hupata Edurenth is promising 6 Umwanamusimbe iliso pansi Mwanamaskini jicho lake daima chini The destitute won’t be tired to loot for, its eyes always down 7 Ushunta sika ukinuna Mganga hajigangi The physician won’t medicate oneself 8 Tyuti nu Maluka Rafiki pete na Kidole The friend with close intimacy 9 Intiti zaiyenga Mipama Watu kurejea maskani nyakati za jioni Birds retneat to their nests 10 Umukaku ukugula Asiyesikila la The one who is ituwe Mkuu huvujika guu obstinate will suffer for the consequences 11 Ukakumsinga zangu Kufanya usichokiweza Scrutching a cat 12 Inshoke ngila kaulime Katika msafara wa maisha hakuna kurudi nyuma Retreat no surrender 13 Kitengani kina masala ni kitegwa kina masala Fumbo mfumbie mjinga mjanja atalig’amua Riddle for an ignorant person but for the craftman will disclose. Misemo mingine ya kinyiramba ni:-  Impinda ya Mwanangulu umalile umukenki Tafsiri yakeni: - Uzito wa mzinto anafahamu mbebaji  Msekwa washokile ni Ng’ombe Tafsiri yake ni mtu aliyedhadhauliwa alirudi na mifugo. Maana yake usimdharau mtu hujui kesho atapata nini  Musuli wa Mbwa ukukopangwa kinakili upiu Tafsiri yake ni Mchuzi wa Mbwa hunywewa ungali wa moto, maana yake ni vema kuchukua tahadhari mapema kabla halijaharibika jambo Muuzaa ukulegagwa nulekelwa Vitendawili vya Kinyiramba Fanani: Laale laale - Kitendawili Hadhira: Laale - Tega Fanani: Mweli Mukyeko - Mwezi katika kipeyu Hadhira: Masunsu - Maziwa Fanani: Kiite Muntunda - Uweusi Mtunguni Hadhira: Ndalu - Mlenda uliokaushwa

Mifano ya maneno ya Kinyiramba

hariri
  1. Maze, yaani Maji
  2. Nanhi, yaani Mboga
  3. Mhusuli, yaani Mchuzi
  4. Ndelu, yaani Ndevu
  5. Nzila, yaani Njia

Viungo vya nje

hariri

Marejeo

hariri
  • Maho, Jouni & Bonny Sands. 2002. The languages of Tanzania: a bibliography. (Orientalia et africana gothoburgensia, no 17.) Göteborg: Acta Universitatis Gothoburgensis. Pp ix, 428. ISBN 91-7346-454-6

Kitabu hiki kinataja marejeo mengine kama:

  • Dempwolff, Otto. 1914/15. Beiträge zur Kenntnis der Sprachen in Deutsch-Ostafrika. Teil 5: Ilamba. Zeitschrift für Kolonialsprachen, 5, uk.227-253.
  • Yukawa, Yasutoshi. 1989. A classified vocabulary of the Nilamba language. (Bantu vocabulary series, no 5.) Tokyo: Institute for the Study of Languages and Cultures of Asia and Africa (ILCAA), Tokyo University of Foreign Studies.
  Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kinilamba kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.