Kinili

ndege wadogo wa jenasi Vidua katika familia Viduidae ambao wanatokea Afrika tu
Kinili
Dume la kinili mweusi Vidua funerea
Dume la kinili mweusi
Vidua funerea
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Passeriformes (Ndege kama shomoro)
Familia ya juu: Passeroidea (Ndege kama shomoro)
Familia: Viduidae (Ndege walio na mnasaba na mishigi)
Cabanis, 1841
Jenasi: Vidua
Stresemann, 1914
Ngazi za chini

Spishi 10:

Vinili ni ndege wadogo wa jenasi Vidua katika familia Viduidae ambao wanatokea Afrika tu. Wanaitwa fumbwe pia pamoja na spishi nyingine za Vidua. Wakati wa kuzaa madume wana rangi ya nili, lakini wakati wengine wana rangi za majike, kahawia na nyeupe, wenye michirizi miwili kwa utosi. Hula mbegu za manyasi hasa lakini wadudu pia, kumbikumbi aghalabu.

Ndege hawa hawajengi tago lao lenyewe lakini hutaga mayai yao katika matago ya mtolondo, mshigi tombo au mshigi kidari-machungwa (udusio wa kiota, Kiing. brood parasitism). Kila spishi ya kinili inadusia spishi yake ya mtolondo au mshigi. Kinyume na kekeo vinili hawaharibu mayai ya mwenye tago. Huyataga mayai 2-4 kwa kuzidi yaliyomo. Mayai ya vinili ni meupe kama yale ya mwenyeji lakini wakubwa zaidi. Ndani ya domo la makinda inafanana na ile ya makinda ya mwenyeji na dume anaiga wimbo wake.

Spishi hariri

Picha hariri