Kinyiha
Kinyiha (au Kinyika) ni lugha ya Kibantu nchini Tanzania na Zambia inayozungumzwa na Wanyiha. Isichanganywe na Kinyiha cha Malawi wala na Kinyika cha Malawi. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kinyiha iko katika kundi la M20.
Mwaka wa 1987 idadi ya wasemaji wa Kinyiha nchini Tanzania ilihesabiwa kuwa watu 306,000. Nchini Zambia ilikadiriwa kuwa watu 356,000 (1993).
Lugha ya Kinyiha ina irabu 5 na konsonanti 34. Pia, tofauti kati ya irabu fupi na irabu ndefu huleta tofauti za maana.
Maneno
haririBaadhi ya maneno ya Kinyiha na maana yake kwa Kiswahili ni kama ifuatavyo:
- Amafindango - miujiza
- Aminzi - maji
- Abhantu - watu
- Mwakata - za asubuhi (hutumika kusalimia asubuhi au kama hujaonana na mtu kwa muda mrefu sana)
- Mwizya - hutumika kusalimia mama mmeshaonana na mtu mara ya kwanza
- Ena - mwitiko wa salamu
Marejeo
hariri- Krüger, Susanne; Lindfors, Anna-Lena; Nagler, Louise; Woodward, Mark. 2009. "A sociolinguistic survey of the Nyiha and Nyika language communities in Tanzania, Zambia and Malawi." Ilihifadhiwa 19 Oktoba 2011 kwenye Wayback Machine.
- Maho, Jouni & Bonny Sands. 2002. The languages of Tanzania: a bibliography. (Orientalia et africana gothoburgensia, no 17.) Göteborg: Acta Universitatis Gothoburgensis. Pp ix, 428. ISBN 91-7346-454-6
Kitabu hiki cha Maho na Sands kinataja marejeo mengine kama:
- Busse, Joseph. 1960. Die Sprache der Nyiha in Ostafrika. (Veröffentlichungen des Instituts für Orientforschung der Deutschen Akademie der Wissenschaften zu Berlin, Bd 41.) Berlin: Akademie-Verlag. Kurasa 160.
- Yukawa, Yasutoshi. 1989. A tonological study of Nyiha verbs. Katika: Studies in Tanzanian languages (Bantu linguistics, vol 2), uk.481-518. Tokyo: Institute for the Study of Languages and Cultures of Asia and Africa (ILCAA), Tokyo University of Foreign Studies.
Viungo vya nje
hariri- lugha ya Kinyiha kwenye Multitree
- makala za OLAC kuhusu Kinyiha
- lugha ya Kinyiha katika Glottolog
- http://www.ethnologue.com/language/nih
- http://www.african.gu.se/tanzania/weblinks.html Ilihifadhiwa 4 Oktoba 2006 kwenye Wayback Machine.
- http://www.linguistics.berkeley.edu/CBOLD/Docs/TLS.html (tovuti hiyo ina msamiati wa Kinyiha)
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kinyiha kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |