Tortilla
Tortilla (tamka: tor-ti-ya) ni aina ya mkate bapa wa Meksiko unaofanana na chapati. Kwa kawaida hutengenezwa kwa unga wa mahindi lakini siku hizi kuna pia tortilla za ngano.
Wamexiko huandaa mahindi kwa kuyapika katika maji walimotia kiasi cha chokaa na kuikoboa baadaye. Kupikwa katika chokaa kunaongeza lishe ya mahindi kwa sababu ndani yake kuna proteini na vitamini yasiyopokelewa na tumbo la binadamu bila maandalizi hayo.
Sehemu kubwa ya kinyunga cha tortilla huandaliwa siku hizi viwandani na kuuzwa madukani. Kinyunga hicho hukaushwa tena na kusagwa ikiuzwa kwa umbo la unga utakaochanganywa tena na maji jikoni. Tortilla inaandaliwa kwa umbo la kisahani bapa kama chapati na kuokwa juu ya bati joto au mwenye sufuria.
Mboga ya kienyeji pamoja na tortilla ni maharagwe lakini kuna njia nyingi za kuzila.
Wengi wanapenda kula "taco" barabarani ambayo ni tortilla iliyojazwa nyama, kuku au mboga na kukunjwa ikiliwa mikononi.
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Tortilla kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |