Kipanga-kekeo
Kipanga-kekeo | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
| ||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||
Spishi 5:
|
Vipanga-kekeo ni ndege mbua wa jenasi Aviceda katika familia ya Accipitridae. Ndege hawa ni vipanga wanaofanana na kekeo. Spishi zote zina kishungi. Vipanga-kekeo wanatokea misituni kwa Afrika, Asia na Australia. Hula wadudu wakubwa, Orthoptera (nzige na jamii) hasa, mijusi na nyoka, ndege na wanyama wadogo. Hujenga tago lao mtini na jike huyataga mayai 2-5.
Spishi za Afrika
hariri- Aviceda cuculoides, Kipanga-kekeo wa Afrika (African Cuckoo Hawk)
- Aviceda c. batesi, Kipanga-kekeo wa Afrika ya Kati (Central African Cuckoo Hawk)
- Aviceda c. cuculoides, Kipanga-kekeo wa Afrika ya Magharibi (West African Cuckoo Hawk)
- Aviceda c. verreauxii, Kipanga-kekeo wa Afrika ya Kusini (Southern African Cuckoo Hawk)
- Aviceda madagascariensis, Kipanga-kekeo wa Madagaska (Madagascar Cuckoo Hawk)
Spishi za mabara mengine
hariri- Aviceda jerdoni (Jerdon's Baza)
- Aviceda leuphotes (Black Baza)
- Aviceda subcristata (Pacific Baza)
Picha
hariri-
Kipanga-kekeo wa Afrika
-
Black baza
-
Pacific Baza