Kipimo cha mjao
Kipimo cha mjao (pia: kipimo cha ujazo, kizio cha ujazo) ni namna ya kutaja mjao au kiasi cha kiowevu (kwa mfano maji), gesi au vitu vya kumwaga kama unga au nafaka.
Ni pia kipimo cha kutaja nafasi ndani ya chombo, jengo au gimba la kijiometria kwa jumla.
Vipimo vya SI
haririKipimo sanifu cha kimataifa cha mjao ni mita ya ujazo (alama m³) inayoweza kugawiwa kwa vizio vidogo kama vile desimita ya ujazo au sentimita ya ujazo; kwa kutaja mjao wa magimba makubwa ya maji kama vile ziwa au bahari uwingi wake ni kawaida kutumia uwingi wake yaani kilomita ya ujazo.
Kipimo cha kawaida cha kutaja viowevu kama maji, mafuta au kinywaji ni lita inayolingana na desimita ya ujazo.
Vipimo vya kimila
haririKabla ya kuundwa kwa vipimo vya SI kulikuwa na vipimo mbalimbali vya mjao vilivyo tofauti kati ya nchi na nchi.
Vipimo vya Kiingereza
haririHadi leo vipimo vya kiutamaduni vya Uingereza bado vinatumiwa katika nchi zinazotumia lugha ya Kiingereza kama Marekani, Ufalme wa Maungano au Australia na hapo na pale kati ya watu wa nchi zilizokuwa koloni ya Uingereza. Ilhali vipimo vilisanifishwa katika Milki ya Uingereza wakati wa karne ya 19 baada ya Marekani kupata uhuru vipimo viko tofauti kidogo pande zote mbili. Mifumo hii miwli inajulikana kama "imperial units" (Uingereza) na "US customary measurement" (Marekani).
imperial gallon/US gallons | ||||||
---|---|---|---|---|---|---|
|
Mjao (Uingereza) | ||||
---|---|---|---|---|
Kizio | Kifupi | Ufafanuzi | kipimo linganifu cha SI | kipimo linganifu cha Marekani |
Bushell | 8 gal | 36.37 L | 9.606 US gal | |
Peck | 2 gal | 9.092 L | 2.402 US gal | |
Gallon | gal | 4.54609 lita | 1.201 US gal | |
Quart | qt | 1⁄4 gal | 1.137 L | 1.201 US qt |
Pint | pt | 1⁄2 qt | 568.3 ml | 1.201 US pt |
Gill | 1⁄4 pt | 142.1 ml | 4.804 US fl oz | |
Fluid ounce | fl oz | 1⁄5 gill | 28.41 ml | 0.9608 US fl oz |
Fluid drachm | 1⁄8 fl oz | 3.552 ml | 0.9608 US drachm | |
Minim | 1⁄60 fl dr | 59.19 μl | 0.9608 US minim |
Mjao (Marekani) | ||||
---|---|---|---|---|
Kizio | Kifupi | Ufafanuzi | kipimo linganifu cha SI | kipimo linganifu cha Uingereza |
Gallon | gal | 231 cu in | 3.785 L | 0.8327 imp gal |
Quart | qt | 1⁄4 gal | 946.4 mL | 0.8327 imp qt |
Pint | pt | 1⁄2 qt | 473.2 mL | 0.8327 imp pt |
Fluid ounce | fl oz | 1⁄16 pt | 29.57 mL | 1.041 imp fl oz |
Fluid dram | fl dr | 1⁄8 fl oz | 3.6967 mL | 1.041 imp fl dr |
Minim | 1⁄60 fl dr | 61.61 μL | 1.041 imp fl minim |
Vipimo vya Uswahilini
haririWaswahili wa kale kabla ya enzi ya ukoloni walikuwa na mfumo wa vipimo vyao, pia kwa mjao.
Katika biashara walipima hasa mjao wa nafaka. Kipimo cha kimsingi kilikuwa pishi, Pishi 1 iligawiwa kwa visaga 2 au vibaba 4.
Pishi 12 zilikuwa fara 1. Fara 5 au pishi 60 ziliitwa jizla 1, iliyoitwa pia mzo.[1]
Pishi ililingana takriban na lita 2.5 - 3 lakini jinsi ilivyo katika mazingira ya kimila vipimo vilitofautiana kati ya mji na mji au soko na soko.[2]
Marejeo
hariri- ↑ Sehemu hii kuhusu vipimo vya waswahili inafuata maelezo katika kamusi ya Velten, Suaheli Wörterbuch Teil I, Suaheli - Deutsch, Berlin 1910, uk 358 ("pima")
- ↑ Kamusi ya Kiswahili Sanifu inataja kibaba kuwa "kipimo cha ujazo cha takriban gramu 700", kwa hiyo pishi 1 = vibaba 4 = gramu 2800. Haisemi ni gramu za nini; mahindi huwa na gramu 800 kwa lita moja, unga huwa na gramu ~500 kwa lita. Sacleux katika kamusi yake (dictionnaire Swahili Francais, 1939) anataja pishi kuwa sawa na nusu galoni ya Kiingereza yaani takriban lita 2.25. Velten katika kamusi yake (Suaheli Wörterbuch I. Teil, 1910; "pima") anataja pishi kuwa na takriban lita 4 akirejea kibaba kuwa kama lita 1; hapa ni juu mno kwa sababu kibaba kipo chini ya lita 1. Inawezekana ya kwamba tofauti kati ya kamusi zilizotajwa zinatokana na mahali tofauti ambako waandishi walikusanya habari zao.