Charles Joseph Sacleux (18561943) alikuwa padre wa Shirika la Roho Mtakatifu na mmisionari kutoka Ufaransa aliyekaa miaka mingi Afrika ya Mashariki, hasa Bagamoyo. Anakumbukwa kwa utaalamu wake wa lugha na pia utafiti wake juu ya mimea ya Afrika.

Charles Sacleux (1897)

Sacleux alikuwa mmisionari Mkatoliki wa kwanza aliyeandika juu ya Kiswahili. Alitunga sarufi na kamusi ya Kiswahili. Mwaka 1891 alitunga kamusi ya "Dictionnaire Swahili - Français" iliyochapishwa 1939. Mwaka 1909 alitoa "Grammaire des dialectes Swahilis" (sarufi ya lahaja za Kiswahili). Vitabu vyote viwili vilisifiwa na wataalamu.

Alitunga na kutafsiri vitabu kwa Kiswahili akaandika nyimbo za kiroho zinazotumiwa hadi leo katika Kanisa Katoliki.

Alitunga pia kamusi ya Kiswahili cha Komori "Le dictionnaire Comorien-Francais et Francais-Comorien".

Katika kazi yake ya botania alikusanya mimea mingi ya Afrika ya Mashariki na kuieleza akapokea tuzo za kitaalamu kwa utafiti huu.

Tanbihi

hariri


Viungo vya Nje

hariri