Kitanga cha nyota
Kitanga cha nyota ni eneo la utegili wenye joto sana lililo tabaka la juu zaidi la angahewa la nyota, hasa Jua.[1] Ndani ya kitanga mna miundo iitwayo ndimi.
Kitanga cha Jua kiko juu ya angarangi na kinaenea mamilioni ya kilometa kwenye anga-nje. Kitanga kina halijoto kali sana inayopita kelvini 1,000,000, joto zaidi ya uso wa Jua.[2] Ingawa kitanga kina joto zaidi, uso wa Jua ni angavu zaidi kabisa. Kwa hiyo, kwa kawaida kitanga hakionekani duniani, lakini kinaonekana wazi sana wakati wa kupatwa kwa Jua, ambapo uso wa Jua unafunikwa na Mwezi na kitanga kinaanza kuonekana kama miale ya nuru izingirayo Jua.
Marejeo
hariri- ↑ Baldi, Sergio (1976). A contribution to the Swahili maritime terminology (kwa Kiingereza). Istituto Italo-Africano. uk. 33.
- ↑ Aschwanden, Markus J. (2005). Physics of the Solar Corona: An Introduction with Problems and Solutions. Chichester, UK: Praxis Publishing. ISBN 978-3-540-22321-4.
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kitanga cha nyota kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |