Kitomo
Kitomo | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Kitomo kahawia (Zebrasoma scopas)
| ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
|
Vitomo, vyelwende, vitatange, vitogoo au vitubaku ni samaki wa baharini wa jenasi Paracanthurus na Zebrasoma katika familia Acanthuridae wa oda Perciformes ambao wanafanana na kangaja lakini wana pezimgongo na pezimkundu makubwa kama tanga.
Maelezo
haririKama kangaja vitomo wana miiba kwa umbo la vijembe, mmoja kwa kila upande wa msingi wa mkia ("mikia ya miiba"), ambayo ni mikali na hatari sana. Kwa sababu hii, samaki hawa pia wana rangi kali za onyo. Pezimgongo na pezimkundu ni makubwa, katika jenasi Zebrasoma hasa, na yanafanana na tanga. Mdomo mdogo una safu moja ya meno yanayotumika kwa kujilisha na miani. Mdomo wa spishi za Zebrasoma unatokeza sana.
Spishi
hariri- Paracanthurus hepatus, Kitomo Buluu (Palette surgeonfish)
- Zebrasoma desjardinii, Kitomo Pezi-tanga (Red Sea sailfin tang)
- Zebrasoma flavescens, Kitomo Njano (Yellow tang)
- Zebrasoma gemmatum, Kitomo Madoadoa (Spotted tang)
- Zebrasoma rostratum, Kitomo Mweusi (Longnose surgeonfish)
- Zebrasoma scopas, Kitomo Kahawia (Brown tang)
- Zebrasoma velifer, Kitomo Pezi-tanga ya Bahari ya Pasifiki (Sailfin tang)
- Zebrasoma xanthurum, Kitomo Mkia-njano (Yellowtail tang)
Picha
hariri-
Kitomo buluu
-
Kitomo pezi-tanga
-
Kitomo njano
-
Kitomo madoadoa
-
Kitomo pezi-tanga wa Bahari ya Pasifiki
-
Kitomo mkia-njano
Marejeo
hariri- Rashid Anam & Edoardo Mostarda (2012) Field identification guide for the living marine resources of Kenya. FAO, Rome.
- Gabriella Bianchi (1985) Field guide to the commercial marine brackish-water species of Tanzania. FAO, Rome.
Viungo vya nje
hariri- Kitomo kwenye hifadhidata ya samaki Archived 2 Aprili 2019 at the Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kitomo kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |