Kitukang-Besi-Kusini
Kitukang-Besi-Kusini (pia Kibuton) ni lugha ya Kiaustronesia nchini Indonesia inayozungumzwa na Watukang-Besi kwenye visiwa vya Tukang-Besi, Binongko, Tomea, Madu, Bonerate na Karompa. Watukang-Besi wengine wamehamia visiwa vya Taliabu, Mongole, Buru, Sulabesi, Seram, Ambon na Alor. Mwaka wa 1995 idadi ya wasemaji wa Kitukang-Besi-Kusini imehesabiwa kuwa watu 130,000. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kitukang-Besi-Kusini iko katika kundi la Kicelebiki.
Viungo vya nje
hariri- lugha ya Kitukang-Besi-Kusini kwenye Multitree
- makala za OLAC kuhusu Kitukang-Besi-Kusini
- lugha ya Kitukang-Besi-Kusini katika Glottolog
- lugha ya Kitukang-Besi-Kusini kwenye Ethnologue
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kitukang-Besi-Kusini kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |