Kiunguja
Kiunguja ("lugha ya Unguja") ni lahaja ya Kiswahili iliyo lugha ya kawaida kwenye kisiwa cha Unguja, Tanzania. Lahaja hii ilitumiwa wakati wa ukoloni na Kamati ya kimaeneo ya lugha ya Kiswahili kama msingi wa kuunda Kiswahili Sanifu katika Afrika ya Mashariki. [1]