Lahaja za Kiswahili
Kiswahili kimepatikana kwa namna au lahaja mbalimbali.
Wakati wa ukoloni wa Uingereza azimio lilitolewa kutumia Kiswahili cha Unguja kuwa Kiswahili rasmi katika Tanganyika, Kenya na Zanzibar. Waingereza walikitumia pia kama lugha ya polisi na jeshi katika Uganda.
Kati ya lahaja za Kiswahili ni zifuatazo:
- Kiunguja: kisiwani Unguja (Tanzania) - kimekuwa msingi wa Kiswahili Sanifu.
- Kihadimu (Kimakunduchi): kusini mashariki mwa kisiwa cha Unguja (Tanzania)
- Kimrima: eneo la Pangani, Vanga, Dar es Salaam, Rufiji na Mafia kisiwani (Tanzania)
- Kimgao: eneo la Kilwa (Tanzania)
- Kipate: eneo la Pate, visiwa vya pate (Kenya)
- Kipemba: kisiwani Pemba (Tanzania)
- Kimvita: eneo la Mvita au Mombasa (Kenya). Zamani ilikuwa lahaja kubwa ya kisomi ikitungiwa mashairi kuliko Kiunguja.
- Kingozi: kisiwa cha lamu na viungani mwake (Kenya)
- Kibajuni: magharibi mwa visiwa vya pate (Kenya)
- Chimbalanzi: barawa kusini mwa juba (Somalia)
- Kitikuu: katikati mwa kisiwa cha pate (Kenya)
- Kiamu: eneo la Lamu (Kenya)
- Kijomvu: eneo la Jomvu (Kenya)
- Kingwana: Kiswahili cha Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
- Kisiu: eneo la Siu (pwani ya kaskazini ya Kenya)
- Kivumba: kisiwa cha Vumba na kaskazini kwa Tanga (Tanzania)
- Kimtang'ata: Mtang'ata, mkoa wa Tanga (Tanzania)
- Kimafia (Kingome): Mafia (Tanzania)
- Shikomor: Kiswahili cha Komoro
- Shimaore: Shikomor cha Mayotte (Mahore)
- Shindzuani: Shikomor cha Anjouan (Komoro)
- Shingadzija: Shikomor cha Komoro Kuu
- Kimwani: kaskazini mwa Msumbiji na visiwa vya Kerimba
- Chichifundi: kusini mwa PWANI Kwale,Kenya (kando ya fuo za bahari. hususan Gazi, Munje, Funzi, Bodo, Shimoni, Wasini, Mkwiro na Vanga)
- Chimiini: eneo la Barawa, kusini mwa Somalia.