Kiuzbeki

(Elekezwa kutoka Kiuzbek)

Kiuzbeki ni moja ya lugha za Kiturki za mashariki na lugha ya Kiturki yenye wasemaji wengi katika Asia ya Kati.

Enezi la Kiuzbeki: buluu-nyeusi = wasemaji zaidi ya 50%; buluu-nyeupe = wasemaji chini ya 50%

Kwa lugha yenyewe kuna majina "O‘zbek tili" kwa mwandiko wa Kilatini, "Ўзбек тили" (uzbek tili) kwa mwandiko wa kikirili; au "ئۇزبېك تىلى" (o'zbek tili) kwa mwandiko wa Kiarabu.

Wasemaji hariri

Kiuzbeki ni lugha rasmi nchini Uzbekistan ambako kuna wasemaji milioni 21.

Wasemaji wengine wa lugha hii wako Tajikistan (milioni 1.2), Afghanistan (milioni 1), Kyrgyzstan (550,096), Kazakhstan (332,017) na Turkmenistan (317,333).

Mwandiko hariri

Tangu uenezaji wa Uislamu Kiuzbeki iliandikwa kwa herufi za Kiarabu.

Mapinduzi ya kibolsheviki yalileta mwandiko wa Kilatini kati ya 1929 na 1940 kwa kuiga mfano wa Uturuki. Lakini tangu 1940 siasa ikabadilika tena na lugha ikahamishwa kwa mwandiko wa kikirili kama Kirusi.

Tangu uhuru wa mwaka 1991 mipango ilijadiliwa kurudi kwa mwandiko wa Kilatini. Azimio lilifanywa 1995 kutumia alfabeti ya Kilatini. Lakini hadi sasa mwandiko wa Kikirili bado unapatikana. Waislamu wengine wameendelea kutumia herufi za Kiarabu.

Shule zinatakiwa kufundisha miandiko yote mitatu ili vijana waweze kuendelea kusoma maandishi ya miaka ya nyuma.

Viungo vya nje hariri